Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa la kujadili matumizi ya Nishati itokanayo na joto ardhi katika Nchi za Afrika zinazopitiwa na bonde la ufa. Kongamano hilo limeanza leo Oktoba 29, 2014 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt Bilal, kufungua kongamano hilo. 
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya waliohudhuria kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia. 
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo baada ya ufunguzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wakati akiondoka eneo hilo baada ya kufungua kongamano hilo. Picha na OMR
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: