Shirikisho la kandanda Ulimwenguni ( FIFA ) hii leo limetangaza jumla ya majina 23 wa wachezaji wa soka watakaowania tuzo ya Mchezaji bora wa FIFA " Ballon d'Or " kwa mwaka 2014. 

Hata hivyo kabla ya mwezi wa 12, majina hayo yatachujwa na kubakizwa majina ya wachezaji 3 ambao ndio wataingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hiyo. 

Mshindi atakabidhiwa tuzo hiyo January 12' 2015 mjini Zurich, Uswis.Majina hayo ya wachezaji na nchi wanazotoka ni kama ifuatavyo:-

Gareth Bale (Wales), Karim Benzema ( Ufaransa ), Diego Costa ( Hispania ), Thibaut Courtois ( Ubelgiji ), Cristiano Ronaldo ( Ureno ), Angel Di Maria (Argentina ), Mario Goetze ( Ujerumani )

Wengine ni Eden Hazard ( Ubelgiji ), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), Andres Iniesta ( Hispania ), Toni Kroos ( Ujerumani ), Philipp Lahm ( Ujerumani ), Javier Mascherano (Argentina ), Lionel Messi (Argentina ).

Pia wamo Thomas Mueller ( Ujerumani ), Manuel Neuer ( Ujerumani ), Neymar ( Brazil ), Paul Pogba ( Ufaransa ), Sergio Ramos ( Hisapnia ), Arjen Robben ( Uholanzi ), James Rodriguez (Colombia), Bastian Schweinsteiger ( Ujerumani ), na Yaya Toure (Ivory Coast).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: