Meneja wa maonesho ya filamu za Kiafrika Arusha(AAFF), Bi.Mary Birdi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza mdhamini wa maonesho hayo kampuni ya Tigo, maonesho yatakayofanyika Septemba 20 mpaka 27 jijini Arusha, kulia kwake Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa Tigo Bw. David Charles.
Meneja wa Mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyancha (aliyesimama) akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha leo wakati wa mkutano kuhusu udhamini wa Tigo maonesho ya AAFF.
Mkurugenzi wa kanda ya Kaskazini wa Tigo, Bw. David Charles akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni ya Tigo kwa maonesho ya filamu za Kiafrika Arusha (AAFF) yatakayofanyika Septemba 20 mpaka 27 jijini Arusha. Kushoto kwake Meneja wa maonesho ya AAFF, Bi. Mary Birdi.
Na Mwandishi Wetu.
Tigo Tanzania leo imetangaza udhamini wake kwama onesho ya filamu barani Afrika yatakayofanyika mkoani Arusha kuanzia Jumamosi wiki hii.
Maonesho hayo ya wiki moja yanayojulikana kama maonesho ya filamu za Kiafrika Arusha (AAFF) yataonesha filamu mbalimbali za wasanii nchini na kimataifa.
Akitangaza udhamini huo kwa waandishi wa habari kutoka ofisi za Tigo Arusha, Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa Tigo, David Charles alisema kwamba udhamini huo wa Tigo katika maonesho hayo ya filamu ni dhamira ya dhati ya kampuni hiyo katika kuendeleza tasnia ya filamu nchini ambayo kwa sasa inatoa ajira kwa maelfu na maelfu wa vijana nchini na kuwainua kimaisha.
“Tasnia ya filamu nchini imebadilika kutoka kuwa tasnia ambayo ina burudisha wapenzi wake na kuwa sekta inayotoa ajira kwa vijana. Tunaamini kwamba AAFF ni fursa nzuri kwa waigizaji na waandaji wa filamu kuonyesha vipaji vyao na kutangaza pia utamaduni wa Tanzania kimataifa,” alisema Charles.
Aliongeza, “Tunaamini kwamba katika kutoa mchango wetu katika mipango kama hii, tasnia ya filamu nchini itakua na hatimaye kufikia kilele chake; kutengeneza nafasi za kazi zaidi kwa vijan aambao wanapenda kuigiza, kuongoza na kutengeneza filamu; pia kuwa kama daraja la kutangaza utamaduni wetu hususan lugha yetu ya Kiswahili. Hii ni namna ya kipekee sana ya kutangaza Tanzania kimataifa.”
Meneja wa maonesho ya AAFF Mary Birdi alisema kwamba hili ni onesho la tatu la mfululizo kutokea tangu kuzinduliwa kwake mwaka juzi huku akitaja maudhui ya mwaka huu kama “Ushirikishwaji wa vijana na mshikamano wakijamii na kitamaduni katika Afrika.”
Maonesho haya yataonesha filamu kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa malengo ya kutoa simulizi za watu wa Afrika kwa namna yao wenyewe itakayowezesha uelewano mzuri zaidi barani Afrika kupitia filamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: