Shirika la Statoil Tanzania limezindua Shindano la biashara iitwayo Mashujaa wa kesho ambayo imelenga katika kuibua ujasiriamali mkoani Mtwara.
Shindano ya Mashujaa wa Kesho inawapa fursa ya kushiriki vijana kuanzia umri wa miaka 18 hadi 25 iliwaweza kushiriki kwa kutoa mawazo ya biashara ambayo hapo baadaye yanaweza kuwa mpango wa biashara (business plan).
Shindano linalenga vijana wa Mkoa wa Mtwara “ Tungependa kuwapa hamasa vijana kushiriki katika fursa zinazojitokeza katika sekta ya gesi iliwawezesha kuona matokeo chanya kupitia biashara mpya katika mkoa huu” hayo aliyasema Ostein Michelsen, Meneja wa Statoil Tanzania.
Mashindano haya yanaenda sambamba na uanzishwaji wa chumba cha kompyuta cha Mashujaa wa kesho ambacho kipo Chuo Kikuu cha Stella Maris Mtwara. Chumba hicho cha kompyuta kimezinduliwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Statoil, Bwana Helge Lund na Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda.
Ndani ya Chumba hicho kuna Kompyuta mpya 15 zilizounganishwa kwenye mtandao wa intaneti na wanafunzi wa washiriki wa mashindano Mtwara zitakazotumika katika kufanyia kazi na kuendeleza mawazo na mipango ya mipango ya biashara.
Mashindano yatapata washindi Mwezi Disemba .Mshindi atapata zawadi ya dola za Kimarekani wa kati washindi wengine wane watapata dola 1000 kila mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments: