Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania. 
Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano. 
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. 
Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono. 
Baadhi ya silaha za kijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu. 
Kikosi cha Wanamaji wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete na wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi. .


Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano. 
Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli . 
Maandamano ya Pikipiki. 
Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano . 
Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu waliorusha njiwa hao nao wametimiza miaka 50 ya Muungano.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: