01/01/2014 - 02/01/2014

Kikongwe mmoja akamatwa uchi wa mnyama chumbani kwa mtu.
AIJULIKANI kuwa ni kigarura au kama kapata matamani ya mwili akaona pengine chumba ile ingefaa kumpatia msaada wa mambo yale.

picha zinajieleza kwa caption zifuatazo.
Pichani anaonekana BI. Kizee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70, ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, alfajiri ya leo Ijumaa Jan 31,2014 ,Polisi wameweza kumnusuru kifo baada ya kudaiwa kukutwa akiwa uchi chumbani kwa mtu akifanya mambo yasiyoeleweka.
Polisi wakiondoka eneo la tukio wakiwa na Shuhuda mmoja aliyedai alikuwa miongoni mwa waliomkurupusha bibi huyo chumbani.
Mashuhuda wa mwanzo wanasema,Bibi huyo amekutwa akitapatapa bila kujua la kufanya huku mwili wake ukiwa Uchi na nguo zake zikiwa pembeni kitendo kinachopelekea kusadikiwa kwamba Bibi huyu ni mchawi wakati wengine walidai tusubiri taarifa ya Polisi na wengine wakisema uwenda kapatwa na matamanio ya kimwili.
Kituo kikuu cha polisi Mjini Bukoba
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri na Manaibu Waziri waliokuwa wakiapisha Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 wakati alipokuwa akiwasili katika hafla hiyo. 
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Jan 30, 2014.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha George Boniface Tuguluvala Simbachawene, kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Jan 30, 2014.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Saning’o Telele, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Jan 30, 2014.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Jan 30, 2014.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri na Manaibu Waziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, Jan 30, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Jan 30, 2014. Picha na OMR
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe(kushoto), akimtabulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka(aliyevaa tai nyekundu) kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen, wakati Waziri Mkuu huyo alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), leo asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe akitoa ufafanuzi wa namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen(wa tatu kutoka kushoto) , wakati alipotembelea Mamlaka hiyo leo asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka. Kulia kwa Waziri Mkuu wa Finland ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na kushoto kwa Waziri Mkuu huyo ni Waziri wa Niashati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Madeni Kipande, akitoa maelezo ya awali ya namna ambavyo Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka hiyo leo asubuhi kuangalia namna Mamlaka hiyo inavyofanya kazi. Aidha, Waziri Mkuu huyo alitembelea Gati namba 1-7.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo. Nyuma ya Waziri Mwakyembe ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
DSC_0014
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.

Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania

Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.

“Ni muhimu kutoa mafunzo kwa vijana wakitanzania wa shule za msingi na sekondari ili wajue kwamba tofauti za rangi na za kidini hazina nafasi ya kutugawa kama binadamu,” amesema Nkhoma.
DSC_0005
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Diamond na Mlezi wao wakimsikiliza Bi. Ledama (hayupo pichani).
DSC_0044
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto.

Alisisitiza kwamba mauaji na mateso ya Auschwitz yalipoteza mamilioni ya watu wasio na hatia na mafunzo haya yanaonyesha chuki na ubaguzi dhidi ya wayahudi na chuki za aina nyingine yoyote hazina nafasi katika ulimwengu wa leo.

Nkhoma amesema kwamba binadamu wote ni sawa na tofauti za kipato au dini au rangi haziwezi tena kujenga chuki dhidi ya binadamu wengine kwa sababu wote kama binadamu tuna haki sawa mbele za mungu.
DSC_0051
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond jijini Dar es Salaam, wakifuatilia sinema maalum ya mauaji ya kambi za mateso ya wayahudi mwaka 1933.

Wakati huo huo, ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto amesema aliona makambi ambako wayahudi, waroma, wasinti, mashoga, wafungwa wa kivita na watu wenye ulemavu walitumia siku za mwisho katika hali ya kinyama.

“Umoja wa Mataifa ulianzishwa kuzuia kila aina hii ya fazaa kutokea tena, lakini bado misiba kuanzia Cambodia hadi Rwanda mpaka Srebrenica inaonyesha kuwa sumu ya mauaji ya kimbari bado inatiririka,” ilisema taarifa hiyo.
DSC_0082
Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond wakisoma baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa.
DSC_0077
DSC_0075
NDEGE ILIYOBEBA MWILI WA MAREHEMU SHEKH ATHUMANI MAGEE




 MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIELEKEA KWENYE NDEGE KUONGOZA WAOMBOLEZAJI
 RUBANI WA NDEGE AKIELEKEZA NAMNA YA KUTOA JENEZA LENYE MWILI WA MAREHEMU
 WAUMUNI WA DINI YA KISSLAMU PAMOJA NA WANANCHI WA MJINI MUSOMA WAKIWA UWANJA WA NDEGE.
 AFIDH WAZIRI MMOJA WA WATU WALIOTOKA NA MWILI WA SHEKH MAGEE DAR AKIAGANA NA RUBANI WA NDEGE
 MWILI UKIONDOLEWA UWANJA WA NDEGE TAYARI KUPELEKWA NYUMBANI
 MKUU WA MKOA WA MARA NYUMBANI KWA SHEKH
 MWILI UKISHUSHWA NYUMBANI
 WAOMBOLEZAJI WAKIWA NYUMBANI

Na Mwandishi Wetu, Mara.

MKUU wa mkoa wa Mara Mheshimiwa John Gabriel Tuppa ameongoza maelfu ya  Wananchi wa Mji wa Musoma kupokea mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa januari 28 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kugua kwa muda na mrefu na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Musoma wakiusubili mwili wa shekh Magee wamesema  wamepata pigo kubwa kutokana na msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza masuala ya dini.

Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa kesho kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.

   INNAH LILLAH WAINNAH ILLAH RAJIUUN
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA SHOMARI BINDA.
Kuna mdada wa miaka 18 Ambae amejifungua binti anaeitwa Maryam kwa bahati mbaya sana mtoto Huyo alipozaliwa hakua na sehemu ya kutoa choo kikubwa hali ya Kua kwamba sehemu hiyo imefunga. Kwa ujuzi wa ma daktari wa muhimbili wamemtoboa hapo ubavuni ili atoe choo kikubwa kwa njia hii. 

Madaktari walimshauri mama mzazi mtoto atafanyiwa operation wa kufungua njia ya choo kikubwa akifika mwaka na nusu. Sasa amefika umri na mama mzazi yupo kwenye hali Duni sana na Hana hela ya kumfanyia mtoto operation huo. 

Nawaomba ndugu zanguni tumsaidie huyu mtoto, kwani hali hii Inaweza kumkuta mtu yoyote. Haya ni Maisha Yake nawaomba mjitokeze kwa Moyo mkunjufu tumsaidie huyu mtoto. 

Kama Una msaada Wowote ule tafadhali nipige mimi apa kwa kutumia number: +255719009004 au Kama upo nje ya Tanzania na umeguswa na hili na unataka kutoa sadaka yako tafadhali Tuma kwenye account yangu ya Barclays: Miss S.Yussuf sort code: 207103 acc: 73049328 pia unaweza kutuma njia ya wastern union. 

Kwa mlikuwepo Tanzania hiyo number yangu ya TIGO PESA. Ahsante sanaa

KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI. MUNGU AWABARIKI SANA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, wakati alipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) wakati walipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) wakati walipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi DAVID MISIME (SACP) anawashukuru wananchi wa kondoa kwa jinsi walivyotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kufanikisha kumkamata mwanamke aliyeiba mtoto mchanga wa siku moja tarehe 20.01.2014 huko katika maeneo ya Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.

Mtoto huyo wa jinsia ya kiume alizaliwa tarehe 19.01.2014 huko katika zahanati ya Thawi. Mama yake mzazi SALMA S/O ZUBERI, mpare, mkazi wa kijiji cha Mwembeni, Kata ya Changaa - Kondoa, alipatwa na matatizo ambayo yalimlazimu kuhamishiwa katika hospitali ya Wilaya ya Kondoa. Wakati mama huyo akiwa anapatiwa matibabu na daktari alibidi mkwe wake aitwaye HADIJA D/O SAID awe anambeba mtoto huyo mchanga. Alitoka naye nje na ndipo akakutana na AMINA D/O JUMANNE MWASI, 22 Yrs, mkazi wa Mningani, Kondoa mjini, alianza akuongea na nyanya wa kichanga hicho cha siku moja baada ya kuzoeana na mwanamke ambaye alijieleza kuwa amelazwa hapo hospitali kutokana na ujauzito aliomba kumshika au kumpakata mtoto huyo.

Mama mkwe huyo alitoka kwenda kutafuta chakula ili mgonjwa atakapomaliza matibabu aweze kula. Baada ya muda alirudi akashangaa kutokumwona mama ambaye naye alikuwa amejifanya ni mjamzito haonekani, alijaribu kumtafuta maeneo mbalimbali na kuuliza watu mbalimbali bila mafanikio ndipo akaamua kutoa taarifa Polisi.

Kwa vile taarifa zilikuwa zimetolewa maenoe mbalimbali wananchi wema walimtilia mashaka mwanamke aliyeiba mtoto na andipo kwa ushiriano mkubwa baada ya kumfuatilia kwa karibu sana Polisi wakafanikiwa kumtia mbaroni tarehe 29.01.2014 wakati alipompeleka motto huyo hospitali ya Wilaya kwani mtoto alianza kuugua.

Baada ya mahaojiano alikubali kuwa alimuiba mtoto huyo na hata uchunguzi wa kitaalamu umebaini mwanamke huyo hajajifungua siku za karibuni.

Ninatoa wito kwa wananchi kutokuamini watu wasiwafahamu kwa asilimia mia, hata kama wanalugha nzuri kiasi gani pia nawatahadharisha wanawake waliokosa watoto kwa muda mrefu utatuzi wake sio kuiba watoto wa watu wengine.

DAVID MISIME – SACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA.
Msanii Mkali wa Sanaa ya uigizaji kutoka Rocky City Mwanza Masele Malekela amesema kuwa atahakikisha sanaa ya uigizaji Mwanza inasimama na kupendwa na wadau wa sanaa uigizaji almaarufu Filamu kwa sababu umechoka na sanaa ya Mwanza kuonekana si kitu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza, Msanii Masele amesema kuwa muda umefika kwa wadau na wapenzi wa filamu kuondoa fikra potovu kwamba wasanii wa Mwanza hawawezi kuigiza muvi nzuri.

Amesema kuwa kumekuwepo na dhana iliyojengeka katika ufahamu ya baadhi ya Wadau kwamba Mwanza hakuna waigizaji wazuri na hivyo kutonunua kazi zao.
Pia ametaja baadhi ya changamoto wanazokutana nazo wasanii wa Mwanza kuwa:
Ø Uchanga wa soko la filamu za Mwanza.
Ø Maeneo ya kufanyia shutingi.

Ø Uelewa mdogo wa Tanzania wa kuamini kila anayefanya sanaa ni Malaya na anakuwa na tabia mbaya.

Ø Sapoti kutoka kwa wadhamini ni ndogo sana hasa hapa jijini Mwanza hivyo inapelekea wasanii wengi wenye vipaji kutoka Mwanza kushindwa kuonesha uwezo wao katika sanaa.

Ø Baadhi ya waongozaji filamu wana tabia mbaya kama kuwataka kimapenzi wasanii wa kike.

Pia ameeleza mafanikio ya ambayo anatarajia kuyapata kuwa ni:
Ø Kuwa msanii mkubwa na kutambulika kimataifa.
Ø Kujenga heshima katika soko la filamu Mwanza.
Ø Kuifanya sanaa kuwa kazi na sio kitu cha ziada kwa msanii.
Ø Kuwainua wasanii wa Mwanza nitakapopata mafaniko kisanaa.

Amewaomba wadau, wapenzi wa Filamu kumkubali na kuwa tayari kupokea Filamu yake Mpya iitwayo RAFAEL ambayo inatarajiwa kuingia sokoni katika sikukuu ya Pasaka.

Kwa yeyote anayemwitaji mpigie kupitia 0767 028400 Zaidi mtazame kupitia www.matukiomedia.blogspot.com
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Meneja Uendelezaji Biashara wa Mwananchi Communications (MCL), Theophil Makunga, aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Waliarwande Lema amesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa makala iliyoandikwa na Mwigamba na kuchapishwa Tanzania Daima ilikuwa ya uchochezi.
Akizungumza na Kajunason Blog muda mfupi baada ya kuachiliwa huru na mahakama hiyo mmoja wa waliokuwa wakituhumiwa katika kesi hiyo Absalom Kibanda amesema `kesi hiyo itakua ni mwanga kwa wanahabari na fundisho kubwa kwa watu wenye nia ovu ya kukandamiza vyombo vya habari.

"Kikubwa tunamshukuru Mungu kwa kuweza kusikiliza sala zetu, hakika kila kitu ni Mungu ndiye anayepanga... Tumeshinda na sasa tupo huru" anasema Kibanda.

Katika kesi hiyo, Makunga ameshtakiwa pamoja na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima ambaye sasa ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda na Mwenyekiti wa zamani wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Kwa pamoja, washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya uchochezi dhidi ya askari wa majeshi ya ulinzi kwa kuchapisha makala kwenye Gazeti la Tanzania Daima ikiwa na maneno yanayodaiwa kulenga kuwashawishi wasiwatii viongozi wao.
Mkurugeni wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa bidhaa za LG, Tanzania, Rajesh Kumar (kulia) na Meneja Masoko wa LG, Shakti Vellu (kulia) wakisaidia kuzindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika duka lao lililoko Quality Center jijini Dar es Salaam.
Bw. Valerian Banda ambaye ni msemaji wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa vifaa vya LG akiongea kuelezea TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania.
Bw. Valerian Banda ambaye ni msemaji wa Kampuni ya Garnet Star akionyesha remote inayotumia sauti katika uendeshaji.
Wageni pamoja na wanahabari wakifuatilia uzinduzi huo.
Mkurugeni wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa bidhaa za LG, Tanzania, Rajesh Kumar  (Kushoto) akieleza machache wakati wa uzinduzi huo.
Mmoja ya wafanyakazi wa Garnet Star akionyesha jinsi TV ambayo unaweza kuitumia kwa matumizi mengine kama ya internet.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambaji vifaa ya LG wakishow love.
Ubora wa Tv hii unaweza kufanya kambo mawili kwa wakati mmoja yani huku unaangalia TV na kutumia internet.
Mkurugeni wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa bidhaa za LG, Tanzania, Rajesh Kumar (kulia) na Meneja Masoko wa LG, Shakti Vellu (kushoto) wakisaidia kuzindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika duka lao lililoko Quality Center jijini Dar es Salaam.
LG imezindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania, TV aina ya OLED inayojikunja ni mwanzo wa burudani ndani ya nyumba. Aina yake ya kujikunja ambayo inaitwa IMAX inatupa uzoefu wa hali ya juu pamoja na kuangalia kwa starehe kubwa.

TV hii mpya aina ya OLED kutoka LG ikiwa na teknolojia ya rangi nne, ambayo kwa mujibu wa kampuni inaongeza pikseli nyeupe kwa rangi nyekundu, kijani na blu kwa mtazamo bora. Itakuwa na screen nyembamba aina ya OLED ambayo ukubwa wake ni 4.3mm. Pamoja na stendi yake ambayo ina vipimo ifuatavyo 1227x799x192mm na uzito wa kilo 17.2.

TV aina ya OLED LG namba 55EA9800 inakuja na idadi ya chaguo ya kuunganisha ambayo ni HDMI port (x4), port ya kusikiliza muziki ( 3.5mm), RF, AV ( composite), port ya muziki, USB 2.0 (x2), USB 3.0 na LAN port.”

TV hii pia ina kitako ambacho ni wazi kama kioo ambacho TV huwa haionekani kama imeungana nacho na TV huonekana kama inaning’inia hewani. Pia TV hii imewezeshwa kuwa na muonekano wa spika tano kwenye kitako chenye LG 55EA9800 zenye uwezo waku toa sauti ya watti 40.

Bwana Rajesh Darji, wa Garnet Star Ltd Distributor wa LG Home Entertainment Products amesema“ Hii TV aina ya OLED inapatikana katika maduka makubwa ya LG na wakala wake.