Mahakama ya Rufaa Kanda ya Dar es Salaam imeridhia hukumu iliyotolewa na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar ya faini ya Sh. Milioni 13 na kumwachia huru staa wa filamu za Kibongo, Msanii Kajala Masanja.
Msanii Kajala sasa ameweza kufanya kweli katika rufaa hiyo iliyofunguliwa na mumewe, Faraji Agostino, ambaye anatumikia kifungo cha miaka mitano katika hukumu ya kesi ya kutakatisha fedha haramu iliyotolewa mapema mwaka huu.
Mapema mwaka huu, ilitolewa hukumu ya msanii Kajala alihukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 213.
Ambapo Msanii Wema aliweza kumlipia kiasi cha shilingi milioni 13.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: