Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Njombe jioni ya leo, Alhamisi, Oktoba 17, 2013, kuanza ziara ya wiki moja kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Njombe.
Miongoni mwa shughuli kubwa ambazo Rais Kikwete atazifanya katika ziara hiyo, ya kwake ya kwanza tokea Njombe kutangaza kuwa Mkoa, ni kuuzindua rasmi Mkoa huo.
Katika siku yake ya kwanza kesho, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, mbali na kuzindua Mkoa wa Njombe pia atazindua Kiwanda cha Chai katika eneo la Ikanga na kuzungumza na wananchi.
Katika ziara hiyo ambako Rais Kikwete atatembelea wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Njombe, Wanging’ombe, Ludewa na Makete, pia atazindua Chuo cha Veta cha Mkoa.
Aidha, Rais atatembelea na kupata taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wa chuma wa Liganga.
Toa Maoni Yako:
0 comments: