Na Abdulaziz Video.
WATU Saba akiwemo askari polisi mmoja wameuawa katika vurugu zinazoendelea wilayani Masasi mkoani Mtwara, zikiwa zimebeba sura ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.
Muuguzi wa zamu hospitali ya wilaya ya Masasi, Mkomaindo Fatuma Timbu amethibitisha kupokea maiti za watu saba.
Majeruhi ambao idadi yao haijajulikana wamekimbizwa hospitali ya misheni ya Ndanda kwa matibabu na hali bado ni tete Vurugu kubwa zilianza majira ya saa 4 asubuhi leo baada ya polisi waliokuwa wakiendesha pikipiki kumgonga mtu na kukataa kutoa ushirikiano,Hata hivyo hoja hiyo ilihamia kwenye gesi na kundi la vijana mara moja walivamia nyumba ya mbunge wa Masasi, Mariam kasembe na kuiwasha moto, pamoja na magari mawili.
Aidha vijana hao walivamia nyumba ya Anna Abdallah na kuiteketeza kwa moto,kabla ya kuivania ofisi ya CCM wilaya na kuichoma moto pamoja na magari matatu.Hasira za wananchi hao zilifika kituo kidogo cha polisi kilichopo Mkuti na kukichoma moto, baadae walichoma moto magari matano ya halmashauri ya wilaya.
Pia walichoma moto ofisi ya elimu ya halmshauri ya wilaya Masasi vijijini, kabla ya kuichoma ofisi ya maliasili.
Polisi kutoka maeneo mbalimbali yandani na nje ya mkoa inadaiwa walitumia risasi za moto na kusababisha vifo vya watu Sita huku polisi akidaiwa kuuawa kwa kupigwa na wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: