Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya maarufu
kama Bongo Fleva aliyepatia makali yake katika taasisi ya kukuza na
kulea ya vipaji ya Tanzania House of Talents (THT), Mwasiti Almas,
amesema kwamba mwaka huu wa 2013 lazima apate mtoto, ingawa hakumtaja
mtu ambaye yupo tayari kuzaa naye, akisema kuwa itabaki kuwa siri
yake.
Mwasiti aliyasema hayo, wakati
akizungumza na wasanii wenzake bila kujua kuwa mahali apokuwapo
kulikuwa na chanzo chetu cha habari, ambapo hata hivyo aliwasihi
maswahiba wake kuificha siri hiyo hadi itakapokuwa tayari.
Mwasiti anayetamba na wimbo wake wa
'Mapito', ameonekana kuwa moto wa kuotea mbali kutokana na kufanya
kazi ya maana na kutishia usalama wa wasanii wenzake wa kike
wanaotamba katika tasnia hiyo ya muziki wa kizazi kipya.
“Hakika mwaka huu lazima nizae maana
nimeshapanga hivyo na nitashukuru kama Mungu atakubali dua yangu hii
nikiamini kuwa ni hatua kubwa zaidi kwa maisha yangu.
“Nimekuwa nikijipanga na kutamani
suala hili litimie katika kipindi cha mwaka huu, hivyo nitashukuru
mno kwa hatua hii,” alisema Mwasiti.
Nyimbo nyingine zilizowahi kuimbwa na
Mwasiti ni pamoja na Kisa Pombe, ambapo pia lengo lake lingine kwa
mwaka huu ni kuifungua rasmi ofisi yao ya wasanii wanaotokea mkoani
Kigoma, huku yeye akiwa kiongozi wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments: