Mchungaji Daniel na Hoyce Mbowe, wanapenda kuwakaribisha wote wanaoongea Kiswahili hapa Ujerumani na marafiki wengine katika ibada ya pili ya Kiswahili itakayofanyika Jumapili hii tarehe 13.01.2013 .

Muda wa Ibada: Saa saba mchana (13:00 hours) hadi saa tisa mchana ( 15:00 hours).

Mahali: Evangelischen Friedenskirchengemeinde Bonn

Anuani: Franz-Bücheler-Straße 10
53129 Bonn

Ibada hii ya Kiswahili itakuwa ikifanyika kila Jumapili ya pili ya kila mwezi, ibada ya Kwanza ilifanyika tarehe 9 mwezi uliopita na kuhudhuriwa na watu wengi.

Mawasiliano: dmbowe@hotmail.com or hoycembowe@hotmail.com

Wote mnakaribishwa: Karibuni tumwabudu na tumsifu Mungu wetu.

Maelezo ya Picha
Picha ya kwanza : Mchungaji Daniel Mbowe (nyuma) na na mbele ni dada Eva Machangu wakati akisoma somo katika ibada iliyofanyika hivi karibuni.
Picha ya pili: Mchungaji Hoyce Mbowe akitoa mahubiri katika ibada ya kwanza iliyofanyika Bonn, Ujerumani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: