Ukweli ni kwamba ndoa nyingi za Kikristo zinavunjika kutokana na tatizo hili. Je, hakuna haja ya kuitisha mjadala wa kitaifa? Taifa letu linaangamia kwa kukosa maarifa.

Hivi upungufu wa nguvu za kiume ni nini? Kifupi ni mwanamume kutokuwa na uwezo wa kutoa mbegu bora zenye uwezo wa kutungisha mimba, au kutosimama kwa uume.

Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya wanandoa nchini wanakabiliwa tatizo hili. Kwa hiyo, mabango ya waganga yaliyopo barabarani hayajapunguza kabisa tatizo hilo.

Hawa watu wanatibu watu au majini? Hapo ndipo kiini cha makala haya. Sababu kubwa ya ongezeko la wenye matatizo haya ni kwamba dawa nyingi zinazodaiwa kuponya tatizo hili hazina viwango vya kuitwa dawa, bali ni vichocheo tu kwani kinachopigiwa chapuo huwa ni kumudu tendo kitandani na si nguvu asilia.

Waganga wengi wameelekeza nguvu zao huko na ni hapo ndipo janga hili la kitaifa linapoota mizizi.

Ukweli ni kwamba upungufu wa nguvu za kiume hauondolewi kwa dawa za kuchochea nguvu wakati wa tendo. Hizi zina madhara makubwa na mara kadhaa husababisha vifo kwa wanamume wengi wakiwa ‘guest’ na vimada wao kwani hulipua moyo.

Ni lazima kiini cha tatizo hili kichunguzwe na tiba stahiki ipatikane. Kinyume cha hapo, janga hili linaweza kugeuka na kuwa dubwana kubwa la kutumaliza.

Matatizo ya nguvu za kiume huchangiwa na kuugua kwa muda mrefu, ugonjwa wa kisukari, kuvaa nguo za kubana sana, mionzi ya simu, kompyuta na mengineyo. Pia dawa za kuua wadudu huleta tatizo hili kwani zina viambata sumu viitwavyo ‘estrogen’, matatizo ya kisaikolojia, kupiga punyeto kwa muda mrefu na kutumia vyakula vyenye kemikali.

Utafiti unasema kuna uhusiano mkubwa sana kati ya upungufu wa nguvu za kiume na kuwa na sumu mwilini zinazotokana na vyakula vyenye kemikali tunavyobugia kwa kupenda au kutokupenda.

Ni kutokana na utafiti huo ndipo dawa bora yenye uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini kwa muda mfupi ikagunduliwa. Hii ikiwekwa kwenye kinywaji chochote chenye kemikali, mara moja hutenganisha sumu iliyomo humo.

Dawa hii pia huleta nguvu za kudumu za kiume, hujenga afya na kuleta nguvu asilia. Hutatua tatizo la nguvu za kiume huku ukiondoa pia tatizo la ugumba na ni vizuri wenye matatizo kama hayo wakatumia vyakula vya protini hasa ya mimea kwani hurutubisha mbegu.

Kuna aina 2 ya vyakula ambavyo vimefanyiwa utafiti na kubaini kuwa ni moja ya vyakula vinavyosaidia kuongeza nguvu za kiume na havina madhara katika engezeko la nguvu za kiume, katika vyakula hivyo vyenye uwezo wa kuongeza nguvu za kiume kiasili ni:

1. TANGAWIZI
- Tangawizi ni moja ya chakula kinachoweza kurejesha nguvu za kiume, unaweza kuichemsha tangawizi na ukatumia kwa kuinywa kama chai Asubuhi, mchana na jioni pia Tangawizi unaweza ukaitumia katika mchanganyiko wa kiasili kwa kutumia habat soda,asali,kitunguu saumu na tangawizi yenyewe. JINSI YA KUTUMIA MCHANGANYIKO HUU: Chukua tangawizi na kitunguu saumu vitwange kisha vichanganye na asali pamoja na unga wa habat soda na uwe unakunywa mchanganyiko huu kwa kutumia kijiko cha chai kimoja kutwa mara 3 kwa muda wa wiki moja na utaona mabadiliko.

2. TIKITI MAJI:
-Chakula kingine kinachosaidia katika upande wa kuongeza nguvu za kiume ni tunda la Tikiti Maji, unaweza ukachukua tikiti lako ukalikata na kutengeneza juice ya Tikiti kisha unakunywa ila sio lazima utengeneze Juice hata lenyewe tu unaweza ukalila. Ila jitahidi kutumia tunda hili hata kila siku kwani linasaidia sana kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

32 comments:

  1. nn maana ya habat soda

    ReplyDelete
  2. Replies
    1. Ety uume wang ni mdogo sana nawezaje kuongeza au ni vitu gn nikitumia vitansaidia visivyokua na mazara baadae

      Delete
  3. Ni darasa la ukwel, vp inaweza ikaxaidia hata kwa wale ambao misuli ya uume imelegea, yan haipo strong sana

    ReplyDelete
  4. Nenda katika maduka yadawazakiarabu, nautapata hiyo habatsoda

    ReplyDelete
  5. Nenda kwwnye maduka yadawa zakiarabu, utapata habatsoda

    ReplyDelete
  6. Habari zenu nilikua naomba hiko kipimo cha asali na tangawizi na habbat sauda unaweka kiasi gani hivo vitu katika asali?asanteni

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  8. je tikiti maji msuli ya uume yaweza kaza

    ReplyDelete
  9. mm natumia dawa za haba soda na nakula tikiti na natumia tangawizi bdo nakuwa sina hamu na ndoa yangu kuna wakati nakuwa na nguvu lakini nikiikaribia na kuwa haiba nguvu nifanye nn hata nipate hamu na ndoa yangu?

    ReplyDelete
  10. Pole ila kwa ushauri wangu jaribu kufanya mazoezi (michezo) mana hata jamaa yangu ilimtokea.

    ReplyDelete
  11. mimi tatzo langu ni kwamba ninapofanya mapenz natumia nguvu nyingi mpaka namwaga muda mwingine simwagi kabisa jambo linalohatarisha ndoa yangu hebu nisaidie hapo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yan tatizo lako ndo langu kama umepata jib nitumie sms nam nijue nin shida no.0759726983

      Delete
  12. kwan hakuna mbadala wa habat soda

    ReplyDelete
  13. Kitunguu swaumu na tangawiz na asali unachanganya kwenye maji ya moto au ya baridi

    ReplyDelete
  14. nimependa somoo

    ReplyDelete
  15. Huo unga wa habat soda unapatikanaje

    ReplyDelete
  16. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  17. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  18. Mwanamke anapata maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa tatizo mini au dawa no IPI?

    ReplyDelete
  19. ushaur mzur sana huo

    ReplyDelete
  20. Dt kanyas mtaalamu wa tiba asili toka tanga anazo dawa mbalimbali kwa kutibu kila aina ya ugonjwa anazo dawa asili za nguvu za kiume..pia anazo za kurefusha uume na kunenepesha uume....anatibu UTI..UGUMBA....KUZIBUA MIRIJA..MTAFUTE KUPITIA 0764839091....DAWA ZOTE NI ZA ASILI

    ReplyDelete
  21. Iko vyema mkubwa nimeipenda sana.

    ReplyDelete
  22. Duh hatari jamani kumbe tatizo hill ni kubwa eee

    ReplyDelete