Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Ndg. Justine
Mwandu akifungua mkutano wa Sita wa Mameneja wa shirika hilo katika
hoteli ya Sea Scape iliyopo maeneo ya Mbezi, Dar es Salaam tarehe 3
Desemba 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bima za Maisha, Bi. Rose Lawa na
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Anne Mbughuni. Kulia kwake ni
Mkurugenzi wa Bima za Mali na Ajali, Ndg Ndugu Kura Kalema
Wakurugenzi pamoja na Mameneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano.
Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mwandu (kushoto) akiwakaribisha wajumbe katika
mkutano. Anayesalimiana nae ni meneja wa bima tawi la Songea Ndugu Moses
Senje akifuatiwa
na meneja mwenzake tawi la Tanga Ndugu Romanus Hokororo na mwisho
meneja wa Iringa Ndg Ally Mohammed.
Kutoka kulia ni Bw. Henry
Machoke, Mkurugenzi wa Masoko, akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa
NIC, Elisante Maleko, na Meneja wa tawi la Ubungo, Segeja Mabula katika
mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: