Wananchi wa Mwanza wakiipokea
treni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL), kwa ujumbe wa Mabango wakatii
treni hiyo ilipowasili Mkoani Hap oleo mchana. Treni hiyo ilisitisha
huduma zake tangu Mwaka 2009, Imeanza safari zake rasmi kwa mabehewa
Sita, likiwemo moja la daraja la Kwanza. Treni hiyo itakuwa ikifanya
safari zake Mara mbili kwa Wiki.
Baadhi ya Abiria wa wanaotumia
usafiri wa Treni ya Shirika la reli Tanzania (TRL), waliotokea jijini
Dar es Salaam ijumaa kuelekea Mkoani Mwanza wakiwa ndani ya behewa la
Daraja la Tatu kama walivyokutwa leo asubuhi .Treni hiyo imeanza safari
zake kutokea Dar kwenda Mwanza.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt.
Charles Tizeba (mwenye suti Nyeusi), akiwa ndani ya Mabehewa ya Treni ya
Shirika la Reli Tanzania (TRL) leo Asubuhi wakati alipoipokea treni hiyo
iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Slaam.Treni hiyo ya kwenda Mwanza
imeanza rasmi Ijumaa kutokea Dar kwenda Mwanza baada ya kusitisha huduma
zake tangu mwaka 2009.
Wananchi wa Mkoani Mwanza
wakipunga mkono kuashiria furaha yao kwa kuanza kwa Safari za Treni ya
Shirika la Reli Tanzania (TRL).Treni hiyo imeanza safari zake ijumaa kwa
kutokea Dar es Salaam kuja Mwanza.
Baadhi ya Abiria wanaotumia
usafiri wa Treni ya Shirika La Reli Tanzania(TRL),wakishuka katika
Stesheni ya Mwanza Leo Mchana kutokea dare s Salaam.treni ilisitisha
safari zake kwenda Mwanza mwaka 2009 na Ijumaa ilianza safari kutokea
Dar kwenda Mwanza.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt
Charles Tizeba, akisisitiza wafanya biashara waliojenga vibanda na
kufanyia biashara karibu na Miundombinu ya Reli katika eneo la stesheni
ya Reli Mwanza mpaka Maeneo ya Mamlaka ya Bandari (TPA), kuhama katika
maeneo hayo kama Sheria ya Reli inavyoelekeza.
Toa Maoni Yako:
0 comments: