Tigo yashika nafasi ya 5 duniani na ya kwanza
Afrika kwa makampuni ya simu katika kujitoa kwa huduma za mitandao
ya kijamii, hii ni kulingana na matokeo yaliyotolewa jana na kampuni
ya ‘Socialbakers’ inayohusika na masoko, ufuatiliaji na upimaji
wa mitandao ya kijamii duniani.
Tigo Tanzania ina wastani wa kujibu wa dakika 24 na kiwango
cha majibu ya 87.49% dhidi ya kiwango cha dakika 520 na kiwango cha
65.50% kiwango cha kujibu, kwa sekta hii. Makampuni au bidhaa ambazo
zinajitoa kwa huduma bora za mitandao ya kijamii zinaonekana kuwa na
huduma bora kwa wateja.
“Tunajivunia kuweza kushika namba 5 bora kwa
operasheni zetu duniani na kuwa bora zaidi kwa Afrika.Hili inaonyesha
wazi juhudi na nguvu tunazoweka ili kuhakikisha kuwa tunaongea
na kuwasikiliza wateja wetu wakati wote, kwa njia inayokwenda na wakati
wa sasa, alisema, Diego Gutierrez Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tigo
Tanzania”.
Huduma za kijamii kwa wateja na vipimo vyake ni pamoja
na idadi ya mashabiki,idadi ya maswali yanayoulizwa na mashabiki wa
kurasa,muda wa majibu,wastani wa muda ambao kampuni inachukua kujibu
maandiko ya watumaji na kiwango cha majibu au asilimia ya wanaopata
majibu kutoka kampuni hiyo.
Kwa sasa Tigo Tanzania imefikisha mashabiki 110,000
wa Facebook na kuwa mtandao unaoongoza kwa kuwa na wafuasi wengi facebook.
Socialbakers ni moja kati ya kampuni kubwa zinazofanya tathmini
ya mitandao ya kijamii duniani na lengo lake kubwa ni kufuatilia na
kupima muonekano ya mitandao, katika kila lengo la mtandao dunia nzima
pale ilipo. Socialbakers pia ni moja kati ya kampuni za kuendeleza masoko
zinazotumiwa na Facebook .
Toa Maoni Yako:
0 comments: