Wasanii wa Safari Lager Wezeshwa kutoka Kampuni ya
Integrated Communications wakicheza wakati wa kuelimisha wakazi wa jijini Arusha Tengeru kuhusu program ya Safari Lager
Wezeshwa awamu ya pili mwishoni mwa wiki.
Wasanii wa Safari Lager Wezeshwa kutoka Kampuni ya
Integrated Communications wakicheza wakati wa kuelimisha wakazi wa jijini Arusha Tengeru kuhusu program ya Safari Lager
Wezeshwa awamu ya pili mwishoni mwa wiki.
Balozi wa Safari Lager Wezesha, Faudhia Mohamed (kushoto)
akiwaelimisha wakazi wa Tengeru jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Balozi wa Saafari Lager Wezesha, Bahati Minja(kulia)
akiwaelimisha wakazi wa Tengeru jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Balozi wa Saafari Lager Wezesha, Khadija Mdee(kushoto)
akiwaelimisha wakazi wa Tengeru jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL)
kupitia bia yake ya Safari Lager kesho inatarajia kuzindua rasmi msimu wa pili
wa programu ya kuwaelimisha wajasiriamali wa jijini Mwanza juu ya “Safari Lager Wezeshwa”.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar Es Salaam jana Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
alisema timu ya Mabalozi 15 wa ya kuelimija jamii imeshawasili jijini Mwanza
tayari kuanza kutoa elimu kwa jamii ya wakazi wa Mwanza hasa wafanyabiashara
ndogo ndogo na wa kati juu ya programu ya Safari Wezeshwa.
Alisema Shelukindo, timu hiyo
ilianzia Mkoani Kilimanjaro na baadae ikahamia jijini Arusha ikielimisha jamii
ya Watanzania juu ya programu hiyo na sasa kesho ni jijini Mwanza ambapo watafanyakazi
katika viwanja vya Igoma Standi kwa siku ya kwanza na siku ya pili watakuwa
viwanja vya Paseansi na baadae watahamia Shinyanga,Kahama na Tanga.
Programu hii ilipata mafanikio makubwa, mwaka jana
iliwawezesha wajasiriamali 54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya
biashara na ruzuku za vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi
milioni mia mbili.
Bwana Shelukindo alisema, “Safari Lager kwa mara ya pili inawaletea wamiliki wa biashara nafasi ya
kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa ruzuku
nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika harakati za
kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaoingia na kufuzu
vigezo vya program hii”.
Aliendelea kusema kwamba, nia hasa ya Safari Lager ni
kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia mafanikio katika
kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii inayowazunguka”. Alifafanua
kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo wadogo na sio
wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya programu hiini
kutoa hamasa kwa wajasiriamali
kote Tanzania ili wajitahidi zaidi
katika shughuli wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze
kufikia ndoto zao. Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama
fedha taslimu kwa watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi
vitakavyomsadia mjasiriamali kulingana na kazi anayofanya.
Shelukindo alimaliza kwa kuwapa
changamoto wajasiriamali kujitahidi zaidi sio tu kwa ajili ya kujishindia
ruzuku za programu ya“Safari Lager
Wezeshwa” lakini kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla. Aliwasihi
wajasiriamali na wafanyabiashara kwa ujumla kutega sikio kwa taarifa zaidi juu
ya usajili na kutembelea website ya www.wezeshwa.co.tz.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kusema, “Tunatoa
pongezikwa wajasiriamali kote Tanzania, Safari Lager inatambua na kuthamini
mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu. Tunatoa shukrani zetu za
dhati pia kwa wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba waendelee kuburudika na bia
hii inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio unaofanya tunawawezesha
wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia
kamili, inayodhihirisha mabingwa!.
Toa Maoni Yako:
0 comments: