KATIBU MKUU
KIONGOZI WA SMZ BW. ABDULLAHAMID YAHAYA MZEE AKITOA
TAARIFA YA TUME KWA WAANDISHI WA HABARI MJINI ZANZIBAR.
---
NA MOHAMMED MHINA, ZANZIBAR
TUME YA
RAIS WA ZANZIBAR YA KUCHUNGUZA CHANZO CHA AJALI YA MELI YA SKAGIT, LEO
IMETOA RIPOTI YAKE KWA WAANDISHI WA HABARI NA KUBAINISHA BAADHI YA
KARORO NA KUTOA MAPENDEKEZO YA HATUA ZA KUCHUKUA KWA WALE WOTE
WALIOHUSIKAKATIKA AJALI HIYO.
AKITOA
TAARIFA YA TUME KWA WAANDISHI WA HABARI MJINI ZANZIBAR, KATIBU MKUU
KIONGOZI WA SMZ BW. ABDULLAHAMID YAHAYA MZEE, AMESEMA TUME IMEBAINI KUWA
TAARIFA ZA IDADI YA ABIRIA WALIOPANDA MELI SIKU YA TUKIO ILIKUWA NI
POTOFU.
AMESEMA
TUME HIYO IMEBAINI PAMOJA NA MAMBO MENGINE, KUWA MELI HIYO ILIKUA NA
IDADI YA ABIRIA 447 WAKIWEMO WATANZANIA 429 NA RAIA WA KIGENI 18 TOFAUTI
NA IDADI ILIYOTOLEWA AWALI NA UONGOZI WA MELI HIYO KUWA ILIKUWA NA
ABIRIA 295 WAKIWEMO WAFANYAKAZI KUMI WA MELI HIYO.
AIDHA
TUME HIYO PIA IMEBAINI KUWA MELI HIYO ILISAJILIWA KINYUME CHA SHERIA NA
HIVYO KUPENDEKEZA MSAJILI WA MELI HIYO BW. SEIF JUMA, KUCHUKULIWA HATUA
KALI ZA KINIDHAMU.
HATA
HIVYO TAARIFA YA TUME HIYO IMETOAUTIA NA TAARIFA ZILIZOKUWA ZIKITOLEWA
NA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA IDADI YA MAITI ZILIZOKUWA ZIKIPATIKANA
SIKU HADI SIKU.
KATIKA
RIPOTI YA TUME HIYO, IMESEMA KUWA WATU 81 WALIPOTEZA MAISHA TOFAUTI NA
TAARIFA ZILIZOKUWA ZIKITOLEWA NA JESHI LA POLISI KUWA HADI KUFIKIA
TAREHE 11/8/2011, IDADI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA ILIKUWA NI 143.
MAITI ZA
WATU 222 ZILIPATIKANA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MWAMBAO MWA BAHARI
KWA UPANDE WA ZANZIBAR NA NYINGINE 21 ZIKAPATIKANA MKOANI TANGA.
HATA
HIVYO BAADA YA KUONEKANA KWA KASORO HIYO, BAADHI YA WAANDISHI WALIKUWA
NA WASIWASI KUWA HUENDA TUME HIYO HAIKUPA TAARIFA KUTOKA POLISI NA
MADAKTARI WALIOFANYA UCHUNGUZI WA MIILI IYA WATU LIYOKUWA IKIPATIKANA
SIKU HADI SIKU TANGU KUTOKEA KWA TUKIO HILO.
TUME
HIYO ILIYOKUWA IKIONGOZWA NA JAJI WA MAHAKAMA KUU MH. ABDRUHAKIM AMEIR
ISSA, PIA IMETOA MAPENDEKEZO KUWA WATU WATANO AKIWEMO MMILIKI WA MELI
HIYO BW.SAID ABDAHAMANI JUMA NA NAHODHA BW. MUSSA MAKAME MUSSA PAMOJA NA
MENEJA MKUU WA KAMPUNI YA SEA GALL INAYOMILIKI MELI YA SKAGIT BW. OMARI
MNKONJE WASHITAKIWE MAHAKAMANI.
WENGINE WANAOTAKIWA KUSHITAKIWA NI NAHODHA WA MELI HIYO BW. MAKAME MUSSA NA MHANDISI WA ZAMU WA MELI HIYO.
MELI YA
MV SKAGIT ILIZAMA TAREHE 17/7/2012 KATIKA BAHARINI KARIBU NA KISIWA
KIDOGO CHA CHUMBE NA KUSABABISHA VIFO NA MANUSURA WA ABIRIA WALIOPANDA
KATIKA MELI HIYO.
Toa Maoni Yako:
0 comments: