Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 45 ya Kampuni hiyo tangu kuanzishwa iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Bw. Israel Kamuzora akitoa hotuba katika hafla ya maadhimisho ya miaka 45 ya Kampuni ya Bima ya Ndege ambapo ameipongeza kampuni hiyo kwa kutoa huduma Bora za Bima na zenye viwango na kuitaka Kampuni hiyo kupanua wigo zaidi kutoa huduma mpaka nje ya mipaka ya Tanzania katika nchi za Kenya na Uganda na baadae hata katika Jumuia ya nchi za Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Ndege Insurance Bw. Amani Ndege akisoma wasifu wa marehemu baba yao ambaye ndio Muasisi wa Ndege Insurance Brokers Casmir Bigacho Ndege.
Dakika Moja ya ukimya kumkumbuka Muasisi wa Ndege Insurance Brokers Marehemu Casmir Bigacho Ndege.
Mgeni rasmi Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Bw. Israel Kamuzora sambamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege waki toast katika hafla hiyo kutakiana afya njema na mafanikiko zaidi ya kampuni hiyo.
Mgeni rasmi Bw. Israel Kamuzora (katikati) wakikata keki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege (kulia) pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo Bi. Renatha Mushi Ndege ikiwa ni kuadhimisha miaka 45 ya tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo ya kutoa Huduma za Bima nchini.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Bw. Israel Kamuzora akizindua nembo mpya ya Ndege Insurance Brokers kwenye hafla ya kutimiza miaka 45 ya kampuni hiyo. Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Dkt. Sebastian Ndege.
Mwanasheria wa kampuni ya Ndege Insurance Brokers Bw. Justin Ndege akikabidhi tuzo kwa mfanyakazi aliyedumu muda mrefu katika kampuni hiyo Bi. Eutrophia Benedict (kushoto). Wanaoshuhudia tukio hilo ni mgeni rasmi na Dkt. Sebastian Ndege.
Mfanyakazi Bora wa Mwaka wa kampuni ya Ngede Insurance Brokers Bw. Haruna Said (katikati) akipozi na Mgeni rasmi Bw. Israel Kamuzora sambamba Dkt. Sebastian Ndege.
Mgeni rasmi Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Bw. Israel Kamuzora akipokea tuzo ya heshima ya kuthamini mchango wake katika kuboresha na kusimamia mamlaka ya huduma za Bima hapa nchini kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Ndege Insurance Brokers Dkt. Sebastian Ndege.
Ushers wakisimamia zoezi la wageni waalikwa kusaini kitabu maalum katika hafla hiyo iliyofanyika usiku wa kumakia leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 45 ya Ndege Insurance Brokers.
Mdau Amo Blaze (kulia) na baadhi ya wageni waalikwa.
Pichani juu na chini ni SKYLIGHT BAND ikota burudani kusindikiza maadhimisho ya miaka 45 ya Ndege Insurance Brokers tangu kuanzishwa kwake.
Mbunge wa Jimbo laKigamboni Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na wadau.
Mkurugenzi wa man Magazine Bw. Dismas Massawe (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Brite Chemicals Ltd. Bw. John Martin.
Mdau Rashid Tenga (suti ya kijivu) na baadhi ya wageni waalikwa.
Mkurugenzi wa Ndege Insurance Brokers Bw. Amani Ndege (katikati), Mwanasheria wa Kampuni hiyo Bw. Justin Ndege (wa pili kushoto), Mdau Haki Ngowi (kushoto) na baadhi ya wageni waalikwa.
Waziri wa Zamani wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Frontline Porter Novelli Bi. Irene Kiwia ambao ndio waandaaji wa hafla ya miaka 45 ya Ndege Insurance Brokers.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Ndege Insurance Brokers Dkt. Sebastian Ndege katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: