Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Brandina Chuwa, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Nov 22, 2012 kwa ajili ya kufungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi  wakati wa ufunguzi wa  Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Nov 22, 2012. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Ofisi ya Takwimu waliokuwa Meza Kuu, baada ya kufungua rasmi Maadhimisho hayo leo. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo baada ya ufunguzi rasmi uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamishna wa Sensa , Hajjat Amina Mrisho Said, wakati akiondoka katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Nov 22, 2012 baada ya kufungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. Picha na OMR
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: