Na Devota Mwachang’a
Hatimaye Beatrice Shimende Kantimbo (48) pichani amefanikiwa kusafiri
kwenda nchini India kutibiwa mguu katika
hospitali ya Apollo, kutokana na michango ya wasamalia wema pamoja na Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Beatrice, aliyeambatana na
Mumewe Emmanuel Kantimbo aliwashukuru sana wale wote walioguswa mara baada ya
kupata taarifa zake, na kuamua kumsaidia kwa pesa, ushauri na kwa sala, pia vyombo vya habari.
Beatrice amesumbuliwa na maradhi hayo kwa takribani miaka 12, vipimo vya
kitabibu vimegundua kuwa ni ugonjwa wa matende (elephantiasis).
Mwanamke huyu alikuwa ni 'mchakarikaji' kweli, aliendesha maisha yake kwa biashara kadhaa wa ikiwemo
biashara ya duka, grosari na saluni ya ususi wa nywele pia aliyekuwa akifanya kazi za ushereheshaji (MC)
kwenye sherehe akifahamika kama MC Kimbaumbau,
Hapa alisimulia namna alivyoanza kuugua…"Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa
kwenye biashara zangu pale Ubungo, kuna kitu kilinichoma hapa (anaonyesh
pajani) maumivu yake yalikuwa mithiri ya sindano, hata hivyo hayakudumu sana
wala hapakuwa na alama yoyote.
"Baada ya dakika chache nikajihisi homa kali. nikaanza kutetemeka
mwili mzima, nikaamua kwenda hospitali ya Neema, hospili ya karibu na mahali
nilipokuwa nikiishi pale Ubungo. Daktari akanipima, akagundua nilikuwa na
malaria.
"Wakati huo mguu haukuonyesha dalili zozote za maumivu wala jeraha.
Malaria ilkuwa kali, nikalazwa kwa muda wa wiki mbili pale hospitali.
Nikaruhusiwa, nikarudi nyumbani na hapo ndipo nilipoanza kuona mguu unavimba.
Kaadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mguu nau unavimba"
Kuanzia mwaka 2010 mguu umezidi kuongezeka kuvimba na maumivu makali
yaliyotokana na kidonda kikubwa kilichosababishwa na kuondolewa kwa sehemu ya
nyama ya mguu wake wa kuume iliyokuwa imeoza.
Anasema: "Baadhi ya madaktari wa Muhimbili walinishauri nikubali
kukatwa mguu. Wanasema ya nyama imeoza na mfupa wa mguu umeharibika. Mimi
sikukukubaliana na ushauri wao kwa sababu baada ya kupigwa X-ray 2007
iligunduliwa tatizo kubwa lilikuwa matatizo kwenye mishipa ya kupitisha maji
kutokana na nyama kuharibika. Sio mfupa.
"Nilikataa kwa imani kuwa nitapona tu. Nikijiangalia nina uwezo wa
kusimama na kutembea isipokuwa tu kinachonipa taabu kwa sasa ni nyama za mguu
zimekua sana kiasi kwamba nikitembea zinagusa mguu wa kushoto" alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments: