Mkurugenzi wa Mawasaliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya(kulia)   akikabidhi  computer kwa  Mkuu wa kitengo cha wodi ya watoto  wanaougua Saratani  kwa Daktari Sulende Kubhodja  wa  hospitali ya Muhimbili , (kati ni) meneja wa jengo la wodi hiyo sista Judica Mwambo. Wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania  walitembelea hospitalini hapo  mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa  waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili

Wafanyakazi wanawake wa Airtel (Airtel Divas) wakikaribishwa na Meneja wa wodi ya watoto wanaougua Saratani katika Hospitali ya Muhimbili sista Judica Mwambo ambapo hao walitembelea hospitalini hapo  mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa  waliolazwa hospitalini
hapo Muhimbili

Mkurugenzi wa Mawasaliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya (wapili kulia) akiongea na mmoja wa watoto  waiolazwa katika hospitali ya Muhimbili mwishoni mwa wiki hii ambapo wafanyakazi wanawake wa Airtel waliamua kutembea watoto wenye kuugua Saratani katika Hospitali hiyo mwishoni mwa wiki hii, akifuwatiwa na Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde. Airtel ilijitolea vitu mbalimabli kwaajili ya hospitali hiyo ikiwemo computer, pamoja sabuni, miswaki, na dawa za meno kwaajili ya wagonjwa hao.

Wafanyakazi wanawake wa Airtel (Airtel Divas) wakiingia na mizigo yao katika wodi wa wagonjwa wanasumbuliwa na maradhi ya  Saratani katika Hospitali ya Muhimbili, wafanyakazi hao walitembelea hospitalini hapo mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa  waliolazwa
hospitalini hapo Muhimbili

Wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
na watoto wanaogua Saratani katika wodi ya Muhimbili walipowatembelea
mwishoni mwa wiki hii ambapo Airtel walitoa misaada mbalimbali ikiwepo
 komputa , sabuni, dawa za mswaki na mahitaji mengine muhimu.
---

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel  kupitia programu yake ya AIRTEL
DIVA imekabidhi misaada mbalimbali kwa wodi ya Watoto wanaougua
maradhi ya Kansa katika Hospital ya Taifa Muhimbili. Ikiwa ni mchango
toka kwa wafanyakazi wanawake wa Airtel kuunga mkono jitihada za
Airtel katika kujitolea kwa jamii.

Vifaa vilivokabidhiwa na wanafanyakazi hao wanawake wa Airtel Diva’s
ni pamoja ma Kompyuta mpya kwaajili ya wodi hiyo, itakayotumika
kutunza kumbukumbu za wagonjwa, pamoja na vifaa mbalimbali vikiwemo
vitendea kazi vitakavyotumika katika usafi kwa wagonjwa  waliolazwa
hospitalini hapo Muhimbili.

Akizungumza Katika wakati wa kukabidhi Misaada hiyo,Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano,amesema kuwa  utoaji misaada
hiyo ni Mikakati thabiti iliyowekwa na kampuni hiyo katika kuhakikisha
inakuwa karibu zaidi na jamii, sambamba na kutambua mchango wao katika
kufanikisha jukumu zima la Biashara katika kipindi cha Mwaka mzima.

Singano amesema kuwa AIRTEL inatambua changamoto mbalimbali
zinazoikabili Wodi ya Watoto wanaougua maradhi ya Kansa,na kubainisha
kuwa Msaada walioutoa hautaishia hapo badala yake watakuwa wakifanya
hivyo mara kwa mara katika Hospitali mbalimbali za ndani na nje ya
Mkoa wa Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano-Airtel Bi Beatrice Singano  Airtel kupitia
mpango wetu wa Diva, ambapo ni mkusanyiko wa wafanyakazi wote wanawake
tumeona ni vyema kusaidiana na wazazi wenzetu kwa kuwapa pole  namna
hii, msaana huu tunaokabidhi leo tunaamini utagusa pia wadau wengine
kuja kuwatembelea watoto na ndugu zetu wanaugua maradhi ya kansa
katika hospital ya Muhimbili na hata zingine kwa lengo la kusaidiana
Tumejionea wenyewe shida wanazopata ndugu zetu na hata wauguzaji hivyo
tunaomba sana wanaweza kujitolea kuja kwa wingi na kuhakikisha
tunasaidiana kwa hali na mali kunusuru maisha ya ndugu zetu
hawa”alisema Bi Singano.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Watoto kutoka Hospital ya Taifa
Muhimbili DOKTA SURENDE KUBOJA,ameishukuru Kampuni ya AIRTEL kwa
msaada walioutoa katika Wodi hiyo na kuyataka Makampuni mengine ya
Kibiashara kuiga mfano uliuoonyeshwa na AIRTEL.

Naye Meneja wa Jengo la Watoto kutoka Hospitalini hapo Bi JULITHA
MBWAMBO amesema kuwa Watoto wanaotibiwa katika Wodi hiyo wamekuwa
wakikabiliwa na Changamoto mbalimbali hivyo Misaada iliyotolewa na
AIRTEL itawasaidia katika kupunguza matatizo mbalimbali  yanayowakabili.

Nao baadhi ya Wazazi waliozungumza wodini hapo wamesema kuwa Watoto
wanaowauguza wanahitaji faraja zaidi katika Maisha yao na kuyaomba
makampuni mbalimbali kufuata nyayo za Airtel kwa kuwatembelea na
kuwafariji zaidi.

Pia ZUWENA LISELE Mzazi anayeuguza nae alisema “maisha ya hospitali
ukiwa unauguza ni magumu sana kwa kuwa hakuna anaekuwa amejipanga
kwaajili ya kukabiliana na changamoto za ugonjwa kwa wakati unapotokea
, hivyo kwa niaba ya wenzangu wote ninawashukuru sana wanawake wenzagu
kutoka Airtel kwa kuliona hili na kuja kutoa pole hii, kwa kweli
tumefarijika.

Airtel Diva ni mpango ulio chini ya wafanyakazi wote wanawake wa
Airtel Tanzania wenye lengo la kuwaweka  pamoja kujadili changamoto
mbalimbali za kijamii na kuzitolea ufumbuzi kwa lengo la kuimarishana.

Airtel Diva pia wanalengo la kuhakikisha wanatoka nje ya mazingira ya
kazi na kuhudumia jamii kwa hali na mali ili kutatua changamoto
mbalimbali zikiwemo kuchangia Afya, pamoja na kuelimisha moto wa kike
na jamii kwa ujumla kutambua haki zao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: