Waziri
wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea taarifa ya kutoka kwa
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw Bernard Mbakileki Wizarani Leo. Kamati
hiyo ya watu wanane iliundwa tarehe 27 Agosti 2012 kwa ajili ya
kuchunguza utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Waziri
wa Uchukuzi ameiahidi Kamati kuwa kila kipengele walichoshauri kwenye
ripoti hiyo kitachukuliwa hatua na Mpaka Disemba mwaka huu
Utekelezaji wa Mapendekezo ya ripoti yatakuwa yamekelezwa yote.
Waziri
wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa waandishi wa
Habari (hawapo Pichani)baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya watu
wanane aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka
ya Bandari Tanzania(TPA). Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa
mapendekezo yalioandikwa kwenye ripoti hiyo yatafanyiwa kazi na kila
aliyehusika na ubadhilifu atachukuliwa hatua.
Mwenyekiti wa kamati ya ya uchunguzi wa utendaji kazi wa
Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA),Bw Bernard Mbakileki akisistiza
jambo kwa Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi,Taasisi zilizo chini ya
Wizara na waandishi wa Habari(hawapo Pichani),wakati wa kukabidhi
ripoti waliyoiandika kwa Waziri wa Uchukuzi na kuikabidhi leo. Kulia
kwa Mweyekiti wa Kamati hiyo ni Mhe. Mhandisi. Ramo M. Makani. (Mb)
ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati iliyoundwa kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA), Bw. Bernard Mbakileki akionyesha Magazeti mbalimbali
kwa Waziri wa Uchukuzi, Watendaji wa taasisi za Wizara Uchukuzi pamoja
na waandishi wa habari hawapo pichani yaliyokuwa yakiripoti mambo
mbalimbali wakati uchunguzi huo ulipokuwa ukiendelea.
Waziri
wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe akipokea ripoti ya Kamati
iliyoundwa Kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania
(TPA) kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw Benard
Mbakileki, Kushoto kwa Waziri Mwakyembe ni Naibu Waziri wa Wizara ya
Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, na Kushoto kwa Naibu Waziri huyo ni
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omar Chambo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: