Mwalimu Kibaso ambaye anafundisha masuala ya Sauti (Vocal) akiwapa mazoezi ya viungo vijana waliojiunga katika darasa la muziki linaloendeshwa na Tanzania House of Talent (THT) kila mwezi jijini Dar es Salaam. Darasa hili limekuja kutokana na maombi ya vijana wengi wanaopenda kujifunza muziki.
 Vijana wakiwa katika mazoezi ya viungo ambayo yanasaidia kuwafanya wawe na pumzi ya kuimba.
 Kila mmoja akijiachia kwa bidii kufanya mazoezi.
 Akinadada nao hawapo mstari wa nyuma katika kufanya mazoezi.
 Mazoezi ya viungo yanaendelea, ambapo vijana wengi walipendezwa nayp japo ilikuwa ni mara ya kwanza walionekana kuchoka.
Baada ya kumaliza mazoezi ya viungo vijana walirudi darasani kwa ajili ya kupata masomo zaidi, mwalimu Kibaso akiwaimbisha wanafunzi wake.
 Mwalimu Magawa ambaye yeye ni mtaalamu wa Vyombo (Instruments), akimsikiliza mwanafunzi ambaye alipata nafasi  ya kujielezea maisha yake.
 Wanafunzi wakimsikiliza mwalimu Magawa ambaye aliwafundisha mambo mengi likiwemo suala la kujua aina ya muziki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Hili ni darasa zuri sana.Vijana wajifunze kutumia vyombo ili muziki usiwe wa mpito.

    ReplyDelete