JUMLA ya warembo 29 kati ya 30 wanaowania taji la REDDS MISS TANZANIA 2012 leo wameanza ziara rasmi ya kutembelea Vivutio vya Utalii vilivyopo Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Moshi, Arusha na Manyara.
Warembo hao wakiongozwa na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania, wakiwa katika mikoa hiyo watatembelea vivutio hivyo na kuhamasisha jamii ya watanzania kuwa na desturi ya kutembelea vivutio hivyo vyua ndani na kuhamasisha utalii.
Pia warembo hao watapata fursa ya kujifunza vitu mbalimbali kuhusiana na masuala ya utalii. Oktoba 7, warembo hao watatembrelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, katika lango kuu la kupandia Mlima huo la Marangu.
Aidha kwa mujibu wa ratiba hiyo, inaonesha kuwa warembo hao watafanya tamasha la Michezo mjini Arusha kabla ya kuelekea Monduli ambako Oktoba 8 watazuru Kaburi la Waziri Mkuu wa Zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine.
Misosi ni muhimu bwana kwa warembo, hapa wakiwa Korogwe High Way wakipata kitu ile roho inapenda.
Hawa waliamua kushow love kabla ya kupata mlo wao.
Washiriki hawa wa Redds Miss Tanzania 2012 wao walisema waweke Nakadhalika katika Menu yaoo hapo sasa wana fanya mambo.
Kunywa na kutafuna havikukoma na warembo wa Redds Miss Tanzania walijinafasi.
Tabasamu kwa mpigapi na Camera jamani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: