Habari marafiki, Katika kuelekea siku yangu ya kuzaliwa,
yaani October 21, natarajia kufanya yafuatayo.
(1)
Oktoba 6, nitatembelea moja ya kituo cha kulelea
watoto na kuwafariji.
(2)
Oktoba 7, nitatembelea kambi ya wazee huko Kigamboni na kuwafariji.
(3)
Oktoba 13, nitapata wasaha wa kukaa na watoto wa
mtaani wa maeneo mbalimbali waliopo katikati ya jiji, hii ikiwemo kuwa nao kwa
muda wa siku nzima, ikiwemo maeneo ya Posta,Kariakoo, gerezani, Jangwani na
ferri (Hii ni kwa maeneo yote wanapopatikana waoto hawa.
(4)
Oktoba 14, nitakuwa kwenye fukwe za Kigamboni,
na marafiki ambapo pia watakaojumuika siku hiyo watapata kufundishwa namna ya
kuogelea kwenye maji, sambamba na kujiokoa endapo itatokea matatizo.
(5)
Oktoba October 20,nitatembelea Ocean Road
kwenye wodi ya watoto na baadae nitaelekea Muhimbili kwenye wodi ya watoto na
wamama wamama.
…Oktober 21 nitaelekea kanisani na baada ya
hapo ni kufurahia kwa pamoja na marafiki./
Ukiwa miongoni mwa #TEAM ANDREW CHALE#
unakaribishwa sana usisite, kwani Andrew Chale, katika maisha yake hapa duniani
anakutegemea wewe na ameishi miaka yote tokea saa 12, jioni, October 21,1985,
alipozaliwa pale Muhimbili Hospital, mpaka leo hii amekuwa na kufikia hapa
ameishi na wewe.
Kwa pamoja, Andrew Chale ambaye awali
aliishi katika maisha ya taabu ikiwemo ya watoto wa Mtaani, na baadae kuachana
na maisha hayo (Street children-3yrs) na baadae kuja kuishi na watu baki (2yrs)
na maisha ya kujitegemea (7yrs) mpaka sasa muda huu.
Hakika kwa neema zake Muumba sina la
kumrudishia zaidi ni asante, kwani licha ya kuwa na shida na taabu kila kukicha
najikuta maisha yangu yanaongezeka mbali ya kutokuwa na kazi ambayo nalipwa
mshahara, lakini nakula, kunywa,nalala,natembea nacheka na hakika wapo watu
hapo hapo ambao wanalipwa mshahara na malupulupu hawaishi kwa raha wanaomba ni
bora wafe… kwa mimi nasema ASANTE MUUMBA.
Ili kufanikisha hili ukiwa umeguswa na
unahitaji kuungana name kwenye kushiriki ukiungana na na #Andrew Chale team#,
unaweza kuwasiliana ama kuwakilisha mchango wako kupitia namba kwa MP PESA ama TIGO PESA- 0719076376 ama
0767076376.
Pia
kama utakuwa na vitu ikiwemo nguo ama vyombo ambavyo huvitumii unaweza
wasiliana nami ilikuweza kuvikusanya na kuwafikishia watoto na watu
wasio jiweza.
UNAKARIBISHWA SANA.
Toa Maoni Yako:
0 comments: