Balozi wa kampuni ya Glenmorangie, Bwana Niel Hendriksz akizungumza machache na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Vinywaji vya kampuni hiyo.
Balozi wa kampuni ya Glenmorangie, Bwana Niel Hendriksz, amewasili leo hapa Dar es Salaam kwa ziara ya siku mbili ikiwa ni katika ziara yake ya siku tano katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Waandishi wa habari wakisoma ripoti za kampuni hiyo.
Balozi wa kampuni ya Glenmorangie, Bwana Niel Hendriksz, amewasili leo hapa Dar es Salaam kwa ziara ya siku mbili ikiwa ni katika ziara yake ya siku tano katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Dhumuni la ziara yake ni kuwa zawadia
wanywaji wa Glenmorangie pamoja na kuwaelimisha na kujenga uelewa
kuhusu utumiaji wa vinywaji vya Glenmorangie katika ukanda huu wa
Afrika Mashariki.
Glenmorangie inafahamika kama kinywaji cha
wiski pekee ya kutoka Skotland (Single Malt Scotch Whiskey) tamu na
inayopendwa zaidi duniani. Ikiwa imejijengea umaarufu kama mojawapo
ya wiski za awali kabisa, hasa kwa kuweza kuchanganya mbinu za
kitamaduni pamoja na ugunduzi mpya wa kisasa kujitengenezea jina lake
maarufu la ‘Unnecessarilly well made’, imekuwa moja ya wiski
pendwa zaidi hapa nchini.
Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini,
Hendriksz atakutana na wapenzi wa wiski katika matukio mbalimbali
maalumu ikiwemo chakula cha mchana katika hoteli ya Dar Es Salaam
Serena ambayo itawapa wapenzi wa Glenmorangie nafasi ya kuonja aina
mbalimbali za wiski kutoka Glenmorangie.
PiaHendriksz anatarajiwa kutoa mafunzo maalumu kwa baadhi ya wahudumu kutoka katika bar
kubwa ambayo yatagusa sio tukatika uchanganyaji sahihi wawiskiza
Glenmorangie bali pia historiafupinaainatofautiza Glenmorangie.
Lengokuu la
mafunzo hayo nikuwapa wahudumu ujuzi utakao wawezesha kutoa huduma bora
naya kipekee kwa wateja wao wakati wakiburudika na Glenmorangie kwenye bar au
hotel wanazozipendelea.
Balozi huyo pia anatarajiwa kupita katika
sehemu mbalimbali zinazouzwa Glenmorangie kujibu maswali kutoka kwa
umma pamoja na kuwapa aina tofauti ya kinywaji hicho wale ambao
hawajawahi kuonja kinywaji hicho.
Lakini kikubwa zadi kinachosubiriwa katika
ziara hii ni tukio litakalofanyika jumanne usiku katika hoteli
yaHyatt Regency ambapoHendriksz atafanya sherehe maalumu ya kuonja na
kulinganisha vinywaji vya Glenmorangie.
Huku kukiwa na nafasi ishirini tu kwa nchi
nzima kuhudhuria sherehe hiyo, uhitaji baina ya wapenzi wa
Glenmorangie kuhudhuria umekuwa mkubwa sana. Uonjaji rasmi wa
kinywaji cha Glenmorangie utajumuisha kuonja ladha iliyokomaa vema ya
vichanganyishi vya Glenmorangie huku ukipitia katika ladha tofauti
tofauti, harufu pamoja na vionjo mbalimbali vinavyoikamilisha
Glenmorangie ikifuatiwa na chakula cha jioni maalumu kinachoendana
sambamba na Glenmorangie.
Zoezi hili limebuniwa maalumu ili
kuwafundisha wanywaji wa Glenmorangie namna ambavyo watafurahia zaidi
kinywaji chao cha Glenmorangie.
Ziara ya Hendriksz itamalizika jumatano
asubuhi hapa nchini ambapo ataelekea Nairobi kwamwendelezo wa ziara
hiyo hapa AfrikaMashariki.
Toa Maoni Yako:
0 comments: