Bondia bingwa wa taifa wa kilo 59 toka mkoa wa Tanga Said Mundi "smart punch"amefiwa na baba yake mzazi mzee Abdulrahman Mbaraka nyumbani kwake Zahrau mkoani Tanga. Kifo hicho kilitokea jioni ya jana muda mchache kabla ya mpira wa simba na yanga haujaanza, sababu ya kifo chake cha ghafla inaelezwa ni shinikizo la damu lilitokea kwa muda mfupi na kujaribu kumpeleka katika hospital Bombo na kufia njiani, kwa maelezo ya Said Mundi mwenyewe kwa Ibrahim Kamwe "bigright" ni kuwa baba yake hapo awali hakuwa na ugonjwa huo umekuja ghafla na umemchukua baba. Wanategemea kuzika leo jioni.

Said Mundi anategemea kupanda ulingoni tarehe 26 oktoba 2012 kuzichapa naJ umanne Mohamed raundi kumi kugombania ubingwa wa PST katika uwanja - Tanga. Viongozi wote wa masumbwi kwa pamoja tupo pamoja na Said Mundi katika wakati huu mgumu uliompata na tunashirikiana katika shughuli zima za kufanikisha msiba huu.

Mungu ailaze roho ya mzee Abdi Mbaraka Mundi peponi - Amin
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: