Naibu
waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge (kushoto) akitoa maelekezo kwa
mkandarasi anayejenga barabara inayopita eneo la Jangwani,Kigogo na kuelekea kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha ubungo yenye urefu wa km 6.4 Injinia Abdul Kimaro (kulia kwa naibu waziri) leo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara jijini Dar es salaam.
Eneo la Davis
Corner, Vituka jijini Dar es salaam ambalo baadhi ya wakazi wanalitumia
kutupia taka kinyume cha sheria. Eneo hili litajengwa mzunguko (Round about)
na kuyawezesha magari kupita katika eneo hilo na kupunguza msongamano
wa magari katika eneo hilo katika mikakati inayoendelea ya kupunguza
msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.
---
NAIBU
Waziri wa Ujenzi, Gryson Lwenge amesema serikali kwa
kushirikiana na wakandarasi wa ndani na nje ya nchi watahakikisha
wanakabiliana na tatizo la foleni jijini Dar es Salaam kwa kuimarisha
miundo mbinu ya barabara.
Lwenge
alisema hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kukagua
barabara ya Kigogo yenye kilometa 6.4 na ile ya Jet yenye umbali wa
kilometa 10.
Alisema,
Serikali itahakikisha inapambana na tatizo hilo kwa kuimarisha
miundombinu yote ya barabara licha ya kukabiliwa na changamoto ya
kifedha na wananchi kufungua kesi ya kupinga kubomolewa nyumba zao
kupisha upanuzi huo.
Hata
hivyo, alisema baadhi ya maeneo katika ujenzi wa barabara hizo,
yamesimama kutokana na wananchi kufungua kesi.
Alisema,
barabara hiyo ya Jet yenye kilometa 10 itagharimu zaidi ya shilingi
bil. 12.
Ziara
hiyo iliendelea katika daraja la Kigamboni, barabara ya
Kilwa, mradi wa mabasi yaendayo kasi na barabara ya Mwenge na Tegeta.
Toa Maoni Yako:
0 comments: