Marehemu Kardinal Laurean Rugambwa enzi ya uhai wake.
Kanisa kuu katoliki jimbo la Bukoba ambalo masalia ya mwili wa marehemu kardinali Rugambwa yatazikwa ndani yake.
---
Na Mwandishi Wetu.
Kanisa
katoliki nchini dayosisi ya Bukoba mkoani Kagera, wanajiandaa kuzika
upya masalia ya mwili wa aliyekuwa askofu wa dayosisi hiyo Kardinali
Laurean Rugambwa, aliyefariki mnamo mwaka 1997 katika kanisa kuu la
Bukoba.
Maziko ya
Kadinali Rugambwa yamepangwa kufanyika siku ya oktoba 6 mwaka huu.
Mwili wa askofu huyo wa kwanza nchini na Kardinali wa kwanza mweusi
barani Afrika umezikwa katika kanisa la kwanza mkoani Kagera lililopo
Kashozi kutokana na kwamba kanisa kuu la Bukoba ambalo marehemu aliagiza
kuzikiwa ndani yake lilikuwa katika matengenezo makubwa.
Akizungumza
katika kipindi cha Baragumu Channel ten na baadaye kwenye mkutano na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Askofu msaidizi wa Jimbo la
Bukoba Askofu Methodius Kilaini , amesema wanataka kumzika kardinali
Rugambwa kwa heshima tena katika kanisa alilopenda kuzikiwa kutokana na
kukamilika kwake, lakini kabla ya kuzikwa humo kutatanguliwa na ibada
mbalimbali ikiwa sehemu alikozaliwa, alikobatizwa, sherehe
zitakazoambatana na kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwa kardinali
Rugambwa tarehe 7 mwezi Octoba.
"tuna
alika watu wengi kuhudhuria kwenye tukio hili..., na pia tunakaribisha
michango itakayowezesha kuwa na kitu cha kumkumbuka marehemu kwa mchango
wake.... alisema askofu Kilaini. Naye mmoja wa wajumbe wa kamati ya
maandalizi ya kufanikisha tukio hilo , James Rugemalira, alimwelezea
Kardinali Rugambwa kama mtu aliyetoa mchango mkubwa kwenye jamii ya
watanzania, kuanzia kwenye nyanja za elimu, afya na kiroho.
Marehemu
Kardinali Rugambwa ana mambo mengi ya kukumbukwa na jamii ya watanzania
hususani watu wa mkoa wa Kagera hasa kwa juhudi zake za kupeleka elimu
mkoani humo kwa kuagiza ujengwaji wa shule za msingi na sekondari
ikiwemo shule ya kwanza ya wasichana ya Rugambwa ambayo ujenzi wake
ulikuwa ni mafanikio ya marehemu huyo kuomba msaada wa ujenzi wa shule
hiyo alipohutubia bunge la Ujerumani akiwa mwafrika wa kwanza.
Licha ya
mambo hayo yote kanisa hilo pia liko mbioni kuanzisha mfuko rasmi wa
kumuenzi kardinali huyo mfuko utakaojulikana kwa jina la Kardinali
Rugambwa ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali
za kijamii.
Padre
Laurean Rugambwa aliwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 10 Februari,1952.
Alizaliwa julai 22 1912 na kufariki miaka 15 iliyopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments: