Kimobitel
akiimba wimbo wake aliyeutunga mwenyewe unaojulikana kwa jina la "MGENI" ndani
ya Meeda Sinza Usiku wa kuamkia leo.
Kulia
ni Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki akiimba wimbo mpya wa Kimobitel ndani ya
Meeda Sinza
Banza
Stone AKA Generale akifurahi pamoja na Khadija Mnoga AKA Kimobitel wakati wa
utambulisho usio rasmi wa ujio wa Kimobitel.
Safu
ya wanamuziki nguli wa Extra Bongo walioimba wimbo mpya wa Kimobitel (Mgeni)
wakiongozwa na Ally Choki wa pili kutoka kushoto, wa kwanza kulia ni Rogert Hega
Katapila, anafuatiwa na Banza Stone na Kushoto ni
Kimobitel.
Kimobitel
akiwa na nyuso ya furaha baada ya wapenzi na wadau mbali mbali kumpongeza na
kumpokea kwa mikono miwili ujio wake.
---
Khadija
Mnoga "Kimobitel" hivi majuzi alitangaza rasmi kuihama Bendi yake ya Twanga
Pepeta ambayo aliitumikia kwa miezi kadhaa na kuhamia Extra Bongo, sababu za
kuhama Kimobitel alisema ameamua kurudi Extra Bongo kwa sababu kuna mipango yake
ambayo aliianzisha kwa hiyo amekuja kuimalizia kama wimbo ambao aliwahi kuimba
wakati anaiimbia bendi hiyo unaotambulika kwa jina la "MJINI MIPANGO" kwa hiyo
ameamua kurudi kuja kuikamilisha mipango hiyo.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki amesema KIMO KIMO kama wengine
wanavyomuita atatambulishwa rasmi siku ya Ijumaa ya tarehe 14/09/2012 katika
ukumbi wao wa nyumbani New White House uliyopo Kimara Korogwe jijini Dar es
salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments: