Basi la
kampuni ya Allys Sport Bus linalosafirisha abiria kutoka Dar es
Salaam na Mwanza likiwa limeacha njia na kupinduka baada ya kutokea
ajali inayodaiwa kusababishwa na basi la Shabiby lililokuwa likitokea
mkoani Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu
kuacha njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu
Dodoma-Morogoro ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40
walijeruhiwa mkoani Morogoro.
Basi la
kampuni ya Sumry baada ya kupata ajali katika tukio
Julieth
Ngarabali, Pwani na Hamida Shariff, Morogoro.
---
WATU 11 wanaoaminika kuwa raia wa Kenya wamefariki dunia papo hapo, huku wengine saba wakiwa mahututi baada ya mabasi waliyokuwa wakisafiria kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam kupata ajali katika Mto Wami mkoani Pwani.

Mbali na vifo
hivyo, ajali hiyo pia ilisababisha majeruhi 25 na saba kati yao
waliripotiwa kuwa mahututi na walipelekwa katika Hospitali ya Tumbi,
Kibaha kwa matibabu.
Ajali hiyo
ilitokea katika Kijiji cha Makole, wilayani Bagamoyo wakati abiria
hao ambao ni wanakwaya walipokuwa wakisafiri kutoka Kenya kwenda Dar
es Salaam kushiriki katika tamasha la uimbaji.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri ikihusisha magari manne, mawili kati yake yakiwa ni mabasi hayo yakitokea Kenya na malori mawili ya hapa nchini.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri ikihusisha magari manne, mawili kati yake yakiwa ni mabasi hayo yakitokea Kenya na malori mawili ya hapa nchini.
Tukio hilo
pia lilifunga Barabara Kuu ya Chalinze - Segera kwa zaidi ya saa nane
hivyo abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea na kutoka mikoa ya
Kaskazini ikiwamo nchi ya Kenya kwenda na kutoka Dar es Salaam
kukwama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu alisema raia hao wa Kenya ni waumini wa Kikristo na walikuwa wakielekea Dar es Salaam kwenye tamasha la kwaya.
Ajali ilivyotokea
Mangu alisema awali, mabasi hayo yalikuwa yametokea Segera, huku yakiwa yameongozana na moja ilipofika eneo la Makole ghafla liliyumba na kupinduka kisha kutumbukia kwenye korongo.

Alisema basi
la pili lililokuwa likifuatia nyuma lilipita eneo hilo, lakini baada
ya mita 500, dereva alipigiwa simu na mwenzake kuwa amepata ajali na
wametumbukia korongoni hivyo ikawalazimu kugeuza kurudi nyuma ili
wakawasaidie wenzao.
“Haikuwa rahisi kwa mtu ama gari kuliona haraka hivyo wenzao walipofika hapo nao walipita bila kujua kama kuna gari limeanguka, lakini muda mfupi tu dereva alipigiwa simu na mwenzake akimjulisha kuwa amepata ajali na wametumbukia mtaroni,” alisema Kamanda Mangu.

Alisema baada
ya kugeuza na kurudi eneo la ajali, baadhi ya abiria walishuka ili
kuwasaidia wenzao na wakati wakiwa kwenye harakati hizo, ghafla
lilitokea lori ambalo lililiparamia basi la pili ambalo pia
lilitumbukia kwenye korongo.
Kamanda huyo aliongeza kuwa, wakati basi hilo likigongwa, tayari lilikuwa limegeuzwa kuangalia uelekeo wa Chalinze na kwamba baadhi ya abiria walikuwamo ndani.
Kamanda huyo aliongeza kuwa, wakati basi hilo likigongwa, tayari lilikuwa limegeuzwa kuangalia uelekeo wa Chalinze na kwamba baadhi ya abiria walikuwamo ndani.
Alisema baada
ya lori hilo kuligonga basi hilo, liliendelea mbele kwa kasi na
kugongana uso kwa uso na lori jingine lililokuwa likitokea uelekeo wa
Segera, hivyo kufunga barabara hiyo kwa zaidi ya nane.
“Kwa hiyo
njia ilikuwa imefungwa kuanzia saa 11:00 alfajiri hadi saa 6:30
mchana baada ya askari wetu kufanikiwa kuyaondoa malori hayo kwenye
barabara kuu na sasa (jana) safari zinaendelea kama kawaida,”
alisema Mangu.
Majeruhi
Baadhi ya majeruhi walitibiwa katika Zahanati ya Chalinze na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Tumbi.
Majeruhi
Baadhi ya majeruhi walitibiwa katika Zahanati ya Chalinze na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Tumbi.
Hata
hivyo, RPC Mangu alisema baadaye majeruhi na miili ya marehemu wote
walihamishwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na
maombi ya Ubalozi wa Kenya nchini.
Habari
zilizopatikana jana jioni zinasema kuwa Serikali ya Kenya kupitia
ubalozi wake hapa nchini ilikuwa ikifanya mipango ya kuwarejesha
nyumbani majeruhi na baadaye maiti kwa ajili ya mazishi.
Ajali hiyo ni
kati ya saba ambazo kwa mujibu wa Mangu zilizotokea usiku wa kuamkia
jana na baadhi yake zilisababisha majeruhi zaidi ya 20 katika maeneo
ya Msata, Chalinze na Mbala, wilayani Bagamoyo.
Ajali za Sumry, Allys na
Shabiby ndani ya dk 10
Kutoka Morogoro; watu 45 wamenusurika kufa kwa ajali baada ya mabasi matatu waliyokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka eneo la Mkundi kwa Makunganya nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, katika Barabara ya Morogoro - Dodoma.

Ajali
hiyo ilitokea saa 2:30 asubuhi kwa kuhusisha mabasi matatu, Kampuni
ya Shabiby lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam, Allys
Sport na Sumry yaliyokuwa yakitokea Morogoro kwenda Mwanza.
Baadhi ya majeruhi waliokuwa wakisafiri na basi la Shabiby walisema basi hilo lilianza kuyumba na baadaye kuacha njia kisha kupinduka.
Baadhi ya majeruhi waliokuwa wakisafiri na basi la Shabiby walisema basi hilo lilianza kuyumba na baadaye kuacha njia kisha kupinduka.
Mmoja wa
abiria hao, Rashid Shaaban alisema baada ya basi hilo kupinduka,
ghafla waliona basi jingine la Sumry likiacha njia na kupinduka
wakati lilipojaribu kulipita gari jingine jirani na eneo hilo.
Alisema kuwa
wakati kukiwa na msongamano wa magari katika eneo hilo la ajali, basi
jingine la Allys Sport liliacha njia na kupinduka na hivyo kutokea
ajali tatu katika muda usiozidi dakika 10.
Shaaban alisema baada ya ajali hizo walitokea watu waliokuwa wakijifanya kutaka kutoa msaada, lakini lengo lao lilikuwa ni kuiba mali za majeruhi. Hata hivyo, alisema lengo lao hilo halikufanikiwa kwani muda mfupi baada ya kutokea, askari walifika na kuimarisha ulinzi.

Katika
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, madaktari na wauguzi walionekana
kuzidiwa na wagonjwa kutokana na idadi kubwa ya majeruhi waliokuwa
wakihitaji huduma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alithibitisha kutokea kwa ajali hizo na kusema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa zimetokana na utelezi na mwendo kasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alithibitisha kutokea kwa ajali hizo na kusema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa zimetokana na utelezi na mwendo kasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: