Mwenyekiti wa Bongo move Jacob Stevin
'JB' kushoto akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo juu
ya wizi mkubwa uliotokea hivi karibuni uliofanywa na Kampuni ya Steps
Entatainmenti kwa kushirikiana na wasanii wwenyewe na kudai kuwa
tabia hii ikomeshwa kwa maalamia wa kazi za wasanii kulia ni Msanii
Vicent Kigos 'Ray' na Mwenyekiti wa Shilikisho la Filamu Tanzania
'TAFF' sIMON mWakifwamba.
Msanii wa Filamu Nchini Mohamed Nice
'Mtunisi' kushoto akizungumza na waandishi wa habari wakati
walipokuwa wanatoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuwa wameungana
kupambana na maalamia wa kazi zao za sanaa kushoto ni Mkurugenzi wa
Msama Promotion, Alex Msama na msanii Muhsin Hawadh.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex
Msama katikati akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam baada
ya wasambazaji kuungana na wasanii kwa ajili ya kutoa tamko la
kupambana na malamia wa kazi za sanaa kushoto ni msanii Muhsin
Hawadhi na Mwenyekiti wa Bongo move Jacob Stevin 'JB'
.---
SHIRIKISHO la Filamu nchini(TAFF) kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za
usambazaji wa filamu na kazi za wasanii ‘zimeapa’ kupambana na
maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi ya
wasanii.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni kero kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.
“Umefika wakati kwa
Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali
zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini
kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao”
“Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache ndiyo wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba.
Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.
Alisema Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.
Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka
TRA Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa
kazi hizo kuanzia Januari Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia
Bunge lake kukubalina kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo.
Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi
zao wameungana pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwebnda
kwa haki ili wasanii wapate na wao wawe ni watu wa kusaidi wasanii
kusambaza kazi zao
Toa Maoni Yako:
0 comments: