Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dr. Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua maoni kutoka kwa Mhasibu wa Wizara ya Fedha Abbas Myeto(kulia)kuhusu taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wa umma wanapostaafu. Mkuu huyo wa Nkoa wa Singida aliomba ufafanuzi huyo leo alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua jana mjini Dodoma kutoka kwa watendaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) kwanini kuna utofauti wa ubora katika bendera ya Taifa ya kuweka katika magari kwa viongozi. Mkuu Mkoa huyo aliuliza swali hilo jana alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma. Aliyeshika bendera ndogo ya taifa ni Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akipata maelezo mafupi jinsi Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini [GPSA] inavyosaidia katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyokuwa yakifanyika kupitia ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi za serikali na taasisi zake. Mkuu Mkoa huyo alipata maelezo hayo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia) jana alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.
Mchambuzi wa Mifumo ya Komputya Mkuu Daraja la III kutoka Idara ya Menejimenti ya TEKNOHAMA ya kifedha , Wizara ya Fedha Margethi Ambrosi Nembo (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dr. Parseko Kone (kulia) jana mjini Dodoma jinsi kuingiza mishahara na malimbikizo ya watumishi wa umma kwa kutumia TEKNOHAMA . Mkuu Mkoa huyo alikuwa katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.
Meneja Mawasiliano na Kumbukumbu wa Shirika Hodhi la Mali ya Mashirika ya Umma (CHC) Joseph Mapunda (kushoto) akimpa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dr. Parseko Kone (kulia) jana, jinsi Shirika hilo linavyofanya tathmini ya mashirika ya umma yaliyobinafsishwa na utendaji wa mashirika hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.
Afisa uhusiano na Masoko wa Chuo cha Mipango Dodoma Godrick Ngoli (kulia) akimpa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kulia) jana ,jinsi Chuo hicho kinavyotarajia kutoa kozi mbalimbali zinahusu mazingira ili kukabiliana na changanoto ya ongezeko la watu haoa nchini . Mkuu huyo wa Mkoa alipata maelezo hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitoa changamoto kwa watumishi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma kuwa na mitaala ambayo itawaandaa wananchi kuanzia ngazi ya chini juu ya kuwa na mipango mizuri ya matumzi bora ya ardhi ili kukabiliana na ongezeko la watu nchini. Mkuu Mkoa huyo alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dodoma.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments: