*MNAIGERIA AIBUKA MSHINDI WA KWANZA NA KUCHUKUA USD 3,150/=
 
Mmoja kati ya washiriki wanne walioiwakilisha Tanzania, katika fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur-an, yaliyoshirikisha nchi 13, Omar Abdallah, akisoma Qur-an wakati akishiriki katika fainali za mashindano hayo ya Kimataifa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipohudhuria na kuwa mgeni rasmi katika fainali za mashindano ya Qur-an ya kimataifa, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2012 kuhudhuria fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur-an yaliyoshirikisha  nchi 13, ambapo mshindi alikuwa ni Abdulrahman Salis Ahmad (18) kutoka Nigeria, aliyeshinda kwa jumla ya Pointi 96.12.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: