Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi kikombe Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma
Salum Ally, baada ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa kuwa mshindi wa jumla
katika maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8,
2012, wakati alipokuwa akifunga maonyesho hayo katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha
na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi
mmoja kati ya wajasiliamali wa vikundi vya wakulima, wakati alipokuwa akifunga
rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8,
2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama
Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipowasili kwenye Viwanja vya
Nzuguni mjini Dodoma leo Agosti 8, 2012 kwa ajili ya kufunga rasmi maonyesho
hayo .Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipomwakilisha Rais
Jakaya Kikwete, kufunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane
yaliyomalizika leo Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Tuzo aliyokabidhiwa kwa niaba ya Rais Jakaya
Kikwete ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Rais katika kusimamia na
kuendeleza Kilimo Kwanza, wakati Makamu alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya
Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo
Agosti 8, 2012. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher
Chiza. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Toa Maoni Yako:
0 comments: