Na Mwandishi Wetu.
MDAU wa michezo na aliewahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Villa Squad Fc ya Magomeni jijini Dar es Salaam, Ally Kindoile amejitosa kuwania nafasi ya Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA), unaotarajiwa kufanyika mkoani humo Agosti 28 mwaka huu.

Akizungumza na mwandishi wa kajunason Blog
kwa njia ya simu jana, Kindoile ambaye pia aliwahi kukaimu kwa muda
nafasi Mwenyekiti wa Villa kabla ya kushuka daraja, alisema kuwa,
amechukua uamuzi wa kuwania nafasi hiyo, ili kuinua soka la Mkoa wa
Kilimanjaro na pia kurudisha sifa na heshima iliyokuwepo miaka ya
nyuma kwenye mchezo huo.
Kindoile, alibainisha
mipango yake mikubwa kuwa ni pamoja na kupandisha timu ligi kuu na
kunyakua mataji mbalimbali ikiwamo Taifa Cup.
“Naomba wadau wa michezo
mkoani hapa, kwa pamoja kushirikiana kwa hali na nguvu ili kuleta
maendeleo ya soka, kwa kuwa pamoja tukishirikiana tunayo nafasi ya
kurudisha hali na morali kwa vijana na wanamichezo ndani ya
Kilimanjaro na siku za usoni tupate timu yetu itakayoshiriki ligi kuu
Tanzania Bara,” alisema Kindoile.
Licha ya kuwa mdau wa
michezo, aliwahi kuchezea timu mbalimbali zikiwemo Simba B na Idrisa
Fc, kwa sasa ni mdau mkubwa wa timu ya Kilimanjaro Rangers ya mkoani
Kilimanjaro na amekuwa kwenye mstari wa mbele katika kusaidia vijana
kwenye soka, huku kwa vipindi tofauti alifanikiwa kuipandisha timu ya
Villa Ligi Kuu kwa vipindi viwili ikiwemo msimu 2010-2012.
Toa Maoni Yako:
0 comments: