Na Devota Mwachang’a
Beatrice Shimende
Kantimbo (48) pichani anaomba msaada wa pesa kwa ajili ya matibabu ya maradhi
ambayo vipimo vya kitabibu vimegundua kuwa ni matende
(elephantiasis), ili kufanikisha safari yake kwenda India kwa
matibabu.
Kantimbo anasumbuliwa na
maradhi hayo kwa takribani miaka 12, kwahivi sasa yamemtoa kwenye
mstari wa maisha yake ya kujitegemea na kumfanya awe tegemezi kwa
watoto wake na mumewe ambao hata hivyo kipato chao si cha uhakika.
Kabla ya hapo alikuwa ni
mama 'mchakarikaji' kweli, aliendesha maisha yake kwa biashara kadhaa
ikiwemo biashara ya duka, grosari na saluni ya ususi wa nywele ambapo
yeye mwenywe ni msusi mzuri wa nywele na kwa ucheshi wake na
kujiamini pia alikuwa akifanya kazi za ushereheshaji (MC) kwenye
sherehe kadhaa akifahamika kama MC Kimbaumbau.
Ila kwa sasa, tofauti na
hapo awali alipoitwa MC na mama mchakariji, Kantimbo hawezi kufanya
lolote amebakia ni mama wa kukaa mahali pamoja tu kuanzia asubuhi
hadi jioni.
Kwa uchungu anasimulia
namna alivyoanza kuugua…"Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa kwenye
biashara zangu pale Ubungo, kuna kitu kilinichoma hapa (anaonyesh
pajani) maumivu yake yalikuwa mithiri ya sindano, hata hivyo
hayakudumu sana wala hapakuwa na alama yoyote.
"Baada ya dakika
chache nikajihisi homa kali. nikaanza kutetemeka mwili mzima,
nikaamua kwenda hospitali ya Neema, hospili ya karibu na mahali
nilipokuwa nikiishi pale Ubungo. Daktari akanipima, akagundua
nilikuwa na malaria.
"Wakati huo mguu
haukuonyesha dalili zozote za maumivu wala jeraha. Malaria ilkuwa
kali, nikalazwa kwa muda wa wiki mbili pale hospitali. Nikaruhusiwa,
nikarudi nyumbani na hapo ndipo nilipoanza kuona mguu unavimba.
Kaadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mguu nau unavimba"
Kuanzia mwaka 2010 mguu
umezidi kuongezeka kuvimba na maumivu makali yaliyotokana na kidonda
kikubwa kilichosababishwa na kuondolewa kwa sehemu ya nyama ya mguu
wake wa kuume iliyokuwa imeoza.
Anasema:
"Baadhi ya madaktari
wa Muhimbili walinishauri nikubali kukatwa mguu. Wanasema ya nyama
imeoza na mfupa wa mguu umeharibika. Mimi sikukukubaliana na ushauri
wao kwa sababu baada ya kupigwa X-ray 2007 iligunduliwa tatizo kubwa
lilikuwa matatizo kwenye mishipa ya kupitisha maji kutokana na nyama
kuharibika. Sio mfupa.
"Nilikataa kwa
imani kuwa nitapona tu. Nikijiangalia nina uwezo wa kusimama na
kutembea isipokuwa tu kinachonipa taabu kwa sasa ni nyama za mguu
zimekua sana kiasi kwamba nikitembea zinagusa mguu wa kushoto"
alisema.
Kwa mawasiliano namna ya
kumsaidia piga simu namba 0716 850350, 0784 861031.
Toa Maoni Yako:
0 comments: