Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
imeshauriwa kuungana na Serikali ya Zanzibar katika nia yake ya kununua
meli kubwa kwa ajili ya mizigo na abiria ili kutoa huduma bora ya
usafiri kati ya Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba na kuepusha ajali za
mara kwa mara.
Ushauri
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mipango na Sera wa Chama cha Wakulima
Tanzania Kanda ya Zanzibar Bw. Rashid Yusufu Mchenga, ambapo amesema
kuwa, pamoja na nia nzuri ya Serikali ya Mapinduzi ya kununua meli kama
huku ikijibana kibajeti kwa kiasi kikubwa.
Bw.
Mchenga amesema maafa yaliyotokea kwa siku za hivi karibuni kutokana na
kuzama kwa meli kubwa tatu za abiri za Mv. FATIHI, Mv. SPAICE SLANDER
na MV SKAGIT inatokana na Serikali yenyewe kutokuwa na meli ya uhakika.
Amesema
kuwa matokeo ya ajali hizo yamewagusa karibu Watanzania wote na hivyo
ukimya ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika suala la ununuzi wa
meli kubwa ya Serikali ya mizigo na abiria haileti picha nzuri kwa
wananchi wake wanaotegemea usafiri wa majini kwao pamoja na mali zao.
"Tumechoka kuona ama kusikia Watanzania wanapoteza maisha na mali zao kwa uzembe unaoweza kuepukika". Alisema Bw. Mchenga.
Amesema
kuwa katika kifungu namba 14 cha katiba ya Muungano kinaelezea wazi
kabisa juu ya haki ya kuishi na hivyo ajali za mara kwa mara
zinazokatiza maisha ya Watanzania wenzetu, ni kinyume na sheria hiyo.
Bw.
Mchenga amesema kama ilivyo katika kuimarisha huduma ya usafiri wa
treni za abiria na mizogo kwa mikoa ya Tanzania bara, pia kuna haja
Serikali kuona uwezekano wa makusudi wa kuimarisha usafiri wa abiria na
mizigo majini kwa maana ya bahari, maziwa na mito.
Amesema
usafiri kwenye Maziwa kama Viktoria, Tanganyika, Nyasa na katika vivuko
kwenye mito mikubwa kama Kirombero, Wami, Kagera, Pangani na Ruvu
unaweza kukumbwa na tatizo kama vivuko na madara hayo hayataangaliwa kwa
ukaribu.
Ametilia
mfano meli ya Mv. Liemba inayosafarisha abiiria na mizigo kwenye ziwa
Tanganyika wanaofanya safari kati ya Kigoma nchini Tanzania na Buurundi
kwamba imepitwa na wakati na kuna haja ya Serikali kuona umuhimu wa
kutafuta meli nyingine ili maisha ya wasafiri kwenye eneo hilo yawe ya
uhakika.
"Mimi
naona kuna haja ya Serikali kujitathimini na kujipanga upya kwa
kuangalia vipaumbele na kuimarisha vikosi vyetu vya uokoaji ili kusaidia
kazi za uokozi zitokeapo ajali." Alisema Bw. Mchenga.
Toa Maoni Yako:
0 comments: