Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Geita, Omari Manzie Mangochie amewaasa
wananchi wa jimbo hilo kutoa ushirikiano kwa makalani wa sensa, iliyoanza usiku
wa mkia leo nchini kote.
Akizungumza kwa njia ya simu , Mangochie alisema kuwa, tayari
maofisa mbalimbali wa Sensa wamejipanga kutekeleza majukumu yao ndani ya Wilaya
hiyo na kutaka ushirikiano wa kutosha huku akiwaasa kuachana na vitendo vya
kuchanganya mambo ya siasa, dini na mambo ya msingi.
“Tunaomba ushirikiano
wa kutosha kwa wananchi wa Geita ilikuwasaidia makalani wa sensa
watakaopita sehemu mbalimbali na kupata maelezo ya kila mwananchi, na pia suala
hili si la siasa wala dini ni la maendeleo yetu sote” alisema Mangochie.
Mangochie pia alisema kuwa Wilaya yake inatarajia kupokea
Mwenge wa Uhuru ambao utazindua miradi 15, itakayogharimu kiasi cha Milioni
836.
“Tunatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru kesho na
utazunguka Wilayani na kuzindua miradi
ya 15, yenye thamani ya zaidi ya milioni 836,
hii piautakua hamasa kwa zoezi zima la kuhamasisha sensa ya makazi na
watu” alisema Mangochie.
Aidha, Mangochie aliwataka wananchi kuepuka mambo ya
misuguano kutoka kwa wananchi wanaopitia njia za kisiasa kwani zitaweza kuleta
chuki na baadala yake wawapuuze.
Mwenge huo unatarajiwa kuingia Mkoa huo mpya wa Geita,
katika Wilaya ya Geita ukitokea Sengerema,
Ambapo utazunguka kwa siku hiyo moja na kisha kuingia kweney Wilaya zingine
mpya za Mbogwe, Nyang’wale, Bukombwe na kisha Chato.
Toa Maoni Yako:
0 comments: