Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, mh. Hamad Masud, amejiuzulu kutoka katika nafasi hiyo kufuatia ajali ya Meli ya MV Skagit iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.

Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Insp. Mohamed Mhina amesema kuwa nafasi ya Waziri imechukuliwa na Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani Kusini Pemba Mh. Rashid Seif Sulein. Mheshimiwa Hamad yeye alikuwa ni mwakilishi wa Jimbo la Ole Kaskazini Pemba. Waziri Hamad amechukua uamuzi huo kama sehemu ya kuonyesha uwajibikaji mbele ya umma na kuonyesha mfano kwa viongozi wengine. Kabla ya kujiuzulu, waziri Hamadi alimwandikia barua Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein kumwelezea hatua hiyo na kuomba amruhusu kujiuzulu hatua ambayo Rais ameikubali na kumteua bandala yake.

Katika hatua nyingine, rais ameiteua tume iliyochunguza ajali ya MV Pice ais Slender kucvhunguza chanzo za ajali ya meli ya Skaget.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: