Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Makachero wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, wamemsafirisha kutoka Dar es Salaam kumleta Zanzibar Meneja wa Meli ya Skagit Bw Omari Hassan Mnkonje (50) ili kuunganishwa na watuhumiwa wengine wanaohojiwa na Polisi visiwani hapa.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar ACP Yusuf Ilembo, amesema kuwa meneja huyo wa ambaye ofisi zake zipo Jijini Dar es Salaam ameunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi hiyo.
Meneja huyo alikuwa akishikiliwa na Polisi Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ataunganishwa pamoja na wenzake wengine waliokuwa wakihojiwa na Polisi Visiwani hapa.
Katika hatua nyingine Kamanda Ilembo amesema kuwa watuhumiwa watatu kati ya sita waliokuwa wakihojiwa kuhusiana na tukio hili wamewaachiliwa baada ya kuonekana kuwa hawahusiki katika tukio hilo.
Waliohojiwa na kuachiliwa huru ni pamoja na Fundi wa zamu wa meli hiyo Bw. Hamis Mbarouk Juma(60) ambaye naye alikuwa miongoni mwa manusura katika ajali hiyo.
Wengine walioachiliwa baada ya mahojiano hayo ni Mtaalamu wa Vifaa katika meli hiyo Bw. Ahmed Mashaka Mbarouk(51) mkazi wa Vikokotoni na Mhudumu wa Meli hiyo Bw. Shaibu Godfrey Francis Kanuti(33), mkazi wa Tombondo mjini Zanzibar.
Watuhumiwa wanaoendelea kushikiliwa na Polisi liobaki katika kesi hiyo na ambao watafikishwa mahakamani siku za usoni Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara watakapokamilisha masuala ya mahojiano.
Wakati huo huo, Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wanaoshiriki katika kazi ya utafutaji wa maiti leo wamefanikiwa kuzipata maiti nyingine watano na kufanya idadi ya maiti zilizopatikana hadi sasa kufikia 78.
Miongoni mwa maiti zilizoopolewa leo, moja imetambuliwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Kikosi cha Bendi Zanzibar STG Suleiman Pandu Jape.
Katika Maiti zilizopatikana leo, nne zilikuwa za wanaume akiwemo mtoto mdogo na mmoja ni ya mwanamke ambapo kufuatia kuharibika kwa miili hiyo, Kamishna wa Polisi zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuwa maiti hizo zimefanyiwa mazishi katika makaburi ya pamoja yaliyopo eneo la Kama nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Toa Maoni Yako:
0 comments: