Richard Bukos na Issa Mnally
USIOMBE yakukute!
Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia kisa cha aliyewahi kuwa mpenzi
wa mwanamuziki wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’, Lulu John
(mwenye blauzi nyekundu) anayedai kumfumania mumewe (siyo Mr. Nice),
Risasi Mchanganyiko linafunguka.
Lulu alidai kumfumania bwana’ke
Abdulatif Salum na mwanamke ambaye jina halikupatika kwenye gesti moja
iliyopo Kinondoni B jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.
SINEMA ILIKUWA HIVI
Kwa mujibu wa Lulu, akiwa kwenye mihangahiko
ya kusaka bingo, alitonywa na mtu wake wa karibu kuwa mumewe Abdulatif
yupo kwenye nyumba hiyo ya wageni akiigagadua amri ya sita nje ya
mkataba.
Lulu, baada ya kuthibitishiwa kuwa mumewe anacheza ‘nje
kapu’ ndipo akakodi bodaboda fasta na kuwahi eneo la tukio kwani naye
siyo mgeni wa uwanja huo wa mechi za kitandani.
Alidai kuwa ilimchukua dakika 12 tu kutoka Kijitonyama, Dar anakoishi na mumewe hadi eneo la tukio.
MPAKA CHUMBANI
Aliendelea kusema kuwa baada ya kutimba mahali
hapo alikwenda moja kwa zote hadi kwenye chumba walichojichimbia wawili
hao na kuanza kubamiza mlango huku akipiga mayowe ya kuomba msaada.
WENGINE WADHANI WAMEFUMANIWA
Huku akizidisha kupiga kelele
akitaka kuvunja mlango, ndipo akakatiza stimu za watu wengine waliokuwa
wakilimega tunda tamtam kwenye vyumba vingine ambao walitoka kwa kihoro
wakidhani wamefumaniwa wao.
MUME ATIMKA NA NGUO YA NDANI
Aliendelea kusimulia mkasa kuwa watu
walianza kujaa nje ya chumba hicho ndipo Abdulatif akafungua mlango kwa
kasi na kutimka kama mkizi akiwa na nguo ya ndani pekee kisha akaruka
fensi.
WATU WEWEEE!
Alisema kuwa wakati anachomoka nduki alimgonga
kikumbo Lulu na kumwangusha chini huku akimwacha akigaragara ambapo watu
walikuwa wakimkimbiza wakisema: “Weweee.”
VITA
Baada ya kunyanyuka na Abdulatif kumchomoka hivihivi ndipo vita kuu ikaanza dhidi ya mgoni wake.
ANG’ATWA PUA
Alisema kuwa ngumi za uhakika zilipigwa hadi yeye
(Lulu) akang’atwa pua ambapo alitokwa na damu chapachapa usoni huku
aliyefumaniwa akitafuta njia ya kujisitiri baada ya kuchaniwa nguo na
kubaki mtupu.
Baada ya hali kuwa mbaya, Lulu alisema walitokea
wasamaria wema na kuwatuliza ambapo yeye alikimbilia Kituo cha Polisi
cha Oysterbay, Kinondoni na kumfungulia mgoni wake shitaka la shambulio
la kudhuru mwili lenye jalada la kesi namba OB/RB/12675/2012.
Kwa
mujibu wa Lulu, kitendo cha kumfumania mwanaume huyo kimemuumiza kwani
amekuwa akimtunza kwa hali na mali na hakuweza kuamini kama angeweza
kumsaliti.
Juhudi za kumpata Abdulatif hazikuzaa matunda hadi gazeti hili linakwenda mitamboni hata hivyo zinaendelea.
KWA NINI USIOMBE YAKUKUTE?
Lilikuwa ni tukio la aina yake ambalo
halikuishia pale gesti tu bali liliingia mtaani ambapo vitendo vya
Abdulatif kukimbia akiwa mtupu na Lulu kung’atwa pua viligeuka gumzo na
kila mtu akimuomba Mungu asikutwe na kasheshe kama hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: