Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Mkoani Kilimanjaro, wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo Juni 03, 2012, ambayo yanafanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti aina ya Mroliondo katika eneo la Chem chem ya Maji Njoro,leo Juni 03, 2012, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo Juni 03. 2012, yanayofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha BEP-Environmental Initiatives Consortium, Jensen Siria, kuhusu matumizi na utengezaji wa majiko ya gharama nafuu, wakati alipotembelea katika Banda la kikundi hicho katika maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yaliyozinduliwa Kitaifa na Makamu wa Rais, leo Juni 03, 2012, Viwanja vya  Mashujaa Mkoani Kilimanjaro.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Masoko wa Kundi la Mradi wa i WASH, Kelvin Mwanshilo, wa Shirika la Care, kuhusu vyoo mbadala vya Gharama nafuu, wakati alipotembelea katika Banda la kikundi hicho katika maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yaliyozinduliwa Kitaifa na Makamu wa Rais, leo Juni 03, 2012, Viwanja vya  Mashujaa Mkoani Kilimanjaro.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia mche wa zao la Kahawa wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipokuwa akizindua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea katika Viwanja vya Mashujaa Mkoani Kilimanjaro.
Kikundi cha ngoma za asili cha mkoani Kilimanjaro kikitoa burudani. Picha/Muhidin Sufiani-OMR
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: