Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa (wapili kutoka kulia) akiwakaribisha wageni wake kutoka Zantel Tanzania waliomtembelea ofisini kwake mapema leo. Anayemfuatia ni Mtendaji Mkuu wa Biashara wa Zantel, Ahmed Mokhles, Kulia ni Rashid Tenga, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford. ambapo Zanetl imetoa simu zipatazo 75 kwa Manispaa ya Ilala kwa ajili ya matumizi yao. Mpaka hatua hii hapakuwa na mpangilio wa mawasiliano si tu baina ya wanahalmashauri bali hata kati ya wafanyakazi wa halmashauri na ofisi nyingine. Ilikuwa vigumu kwa wananchi kuwasiliano na maofisa wa hapo manispaa. Sasa, kwa hisani ya Zantel, mawasiliano yamerahisishwa sana. Na hivi karibuni, orodha ya namba za simu itachapishwa ili wananchi waweze kuwasiliana na vitengo na maofisa mbalimbali. Hafla ya makabidhiano imefanyika ofisini kwa meya leo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa (wapili kutoka kulia) akitoa maelezo machache kwa wageni wake.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akipokea msaada wa simu 75 kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Biashara wa Zantel, Ahmed Mokhles kwa ajili ya kusaidia kuboresha mawasiliano katika utoaji huduma kwa wananchi. Kulia ni Rashid Tenga, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford. Hafla ya makabidhiano imefanyika ofisini kwa meya leo .
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akishukuru mara baada ya kupokea msaada wa simu 75 kutoka kampuni ya Zantel.
Toa Maoni Yako:
0 comments: