Zogo lote lilianzia hapa...Askari huyo alipoamuru jamaa wa break down wafunge hilo gari na kulipeleka kituo cha polisi.... Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolosi Kinondoni Jijini Dar es Salaam Konstebo Mfaume Dinya, akipambana na dereva mmoja wa gari yenye namba T266 AZP aina ya Spacio iliyosababisha ajali kwa magari mengine wawili Bw. Gaudes Moshi (25), ambaye alikuwa akikataa yake isifungwe minyororo na kuvutwa kupelekwa Kituo cha Polisi kwa hatua zaidi.
...Ndipo Askari huyo alipomdhibiti jamaa huyo huku akimzonga.
...Askari huyo aliweza kupambana kiukweli ili kujinasua
...hapa alitokea msamalia mwema na kuingilia ugomvi huo..
Gari yenye namba T266 AZP aina ya Spacio iliyosababisha ajali kwa magari mengine wawili.
...hapa jamaa alikuwa akiondolewa eneo la tukio baada ya kuwa amegundua kamera ya Kajunason Blog imenasa tukio hilo.
Ehe...mpaka kieleweke
...Vijana wakiwa wamemzonga askari huyo...
Hatimaye askari huyo alifanikiwa kuamuru break down liifunge gari hiyo na kuikokota.
---
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolosi Kinondoni Jijini Dar es Salaam mwenye namba E7129 Konstebo Mfaume Dinya, jana alilazikika kufanya kazi ya kishujaa kuokoa maisha yake baada ya kuvamiwa dereva mzembe ambaye alikuwa amesababisha ajali.
Askari huyo hata baada ya kuvamiwa na kundi la vijana mara baada ya kumaliza kupima ajali iliyotokea karibu ya eneo la Mbuyuni barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam wananchi hao wakimshambulia kwa kumpiga lakini alihakikisha kuwa maisha yake yanakuwa salama kwa kujikinga zaidi na mashambulizi lakini bila kuleta madhara yoyote kwa waliomvamia na badala yake alihakikisha kuwa anawatia mbaroni baadhi ya wahusika ili awafikishe katika mkondo wa sheria.
Tukio hilo lilitokea pale dereva mmoja wa gari yenye namba T266 AZP aina ya Spacio iliyosababisha ajali kwa magari mengine wawili Bw. Gaudes Moshi (25), kukataa gari yake isifungwe minyororo na kuvutwa kupelekwa Kituo cha Polisi kwa hatua zaidi huku yeye akiwa amelewa chakali.
Baadhi ya mashuhuda wamesema kuwa, pamoja na kwamba Dereva huyo alikuwa amelewa, lakini alikuwa akitafuta ujanja ili aweze kumtoroka askari huyo kama angekubali aiendeshe mwenyewe gari hiyo.
Hata hivyo pamoja na wananchi kutomsaidia askari huyo asichukue hatua kwa dereva aliyesababisha ajali hiyo, lakini askari huyo alipambana kishujaa hadi gari hiyo ikafungwa minyororo na kupelekwa Polisi kituo cha Tegeta kwa hatua zaidi.
Kutokana na hali hiyo, bado serikali kupitia Jeshi la Polisi ina kazi kubwa ya kuwaelimisha wananchi kuwasaidia askari kutekeleza kazi zao kwa kutii sheria bila kushurutishwa.
Wananchi kwa pamoja wanapaswa kutoa ushirikiano kwa Askari Polisi ili kuwawezesha kutekeleza kazi zao katika kutoa huduma kwa jamii na kuacha kuwashambulia pale wanapotekeleza wajibu wao.
Lakini pamoja na mafunzo yake ya kujihami, kwa upande wa Kajunason Blog ambao walishuhudia tukio hilo na kuweza kupata picha, tunatoa pongezi za dhati kwa Askari huyu kwa kazi aliyoifanya usiku wa jana. Big Up.
Toa Maoni Yako:
0 comments: