Mafunzo ya wiki moja kwa makocha
wa mpira wa miguu kwa vituo mbalimbali yameanza leo jijini Mwanza
yakishirikisha zaidi ya makocha 40 wa shule za msingi, za sekondari na
timu za vijana wa mitaani.
Mmoja kati ya makocha wawili
waliotua jijini Mwanza, Alikhan Popat kutoka katika mradi wa kukuza
mpira wa jamii club ya Arsenal ya Uingereza akieleza sababu zao kuwa
nchini na mchakato mzima wa mafunzo hayo.
John Olaleye (raia wa Msumbiji
aishiye nchi Uingereza) akiwa naye ni mkufunzi kutoka mradi wa kukuza
mpira wa jamii club ya Arsenal ya Uingereza amesema kuwa makocha wa timu
ndogondogo jijini Mwanza watapata fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali
ambazo ni msingi muhimu kulea na kukuza vipaji hali itakayo warahisishia
makocha wa timu za madaraja ya juu na Taifa kwa ujumla.
Kwamujibu wa Mkurugenzi wa kituo
cha soka cha Tanzania Sports Academy (TSC) Mutani Yangwe amesema kuwa
mafunzo hayo yanaratibiwa kwa ukaribu na Club ya Arsenal ya nchini
Uingereza na wenyeji TSC yamekuja yakiwa na lengo kuu la kuimarisha na
kuwajengea uwezo Walimu wa timu za soka kwa shule za msingi, sekondari
na timu mbalimbali mitaani.
Wakufunzi John Olaleye na Alikhan
Popat wakijumuika na makocha wa Mwanza kufundisha moja kati ya mbinu
muhimu za awali kwenye mazoezi ya kunyoosha viungo ambapo kwa upande wao
wamesisitiza kuwa kocha mzuri ni yule anayefundisha kwa vitendo.
Makocha wazawa wakijumuika mafunzoni.
Mafunzo yakiendelea kwa makocha wetu...
Hakika soka inatumia lugha moja duniani kote..
Licha ya kubainisha kuwa mafunzo
hayo ni sehemu ya kubadilishana ujuzi mkufunzi mwandamizi wa soka nchini
kutoka kituo cha TSC, Rogashian Kaijage amebainisha kuwa mchakato huo
wa mafunzo utasidia kuwarahisishia hata makocha wa vilabu ngazi za juu
kupokea vipaji vilivyoshiba misingi ya soka na si kupokea wachezaji
mbumbumbu wa misingi ya soka kama ilivyo kwa vilabu vingi nchini hali
inayopelekea taifa kufukuza makocha kila kukicha. Picha/G. Sengo
Blog.
Toa Maoni Yako:
0 comments: