Washiriki wa kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja,safi kabisa tayari kwa kuchuana vikali usiku wa jumamosi Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.Shindano hilo kiingilio chake  kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000/=

Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa katika picha ya pamoja tayari kwa kuchuana vikali usiku wa leo.
---
Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji  Kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2012, yanatarajiwa kufika kileleni jumamosi usiku (Mei 5) ndani ya hoteli ya Kitalii, Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.

Akizungumza leo asubuhi jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka  kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, amebainisha kuwa kila kitu kiko sawa na maandalizi yamekamilika, tayari kwa kumpata mshindi  wa MISS REDD’S ARUSHA CITY CENTRE 2012 usiku wa jumamosi  kati wa Walimbwende 20 watakaoshiriki.

Bi. Upendo Simwita amesema kuwa Warembo wote wenye mvuto na wenye vigezo stahiki wako tayari kwa shughuli moja tu usiku wa jumamosi,anaongeza kuwa warembo hao wana ari kubwa ya ushindani, na kwamba kuna uwezekano mkubwa muwakilishi wa Miss Tanzania 2012 akatokea kwenye kitongoji hicho.

“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20,ambao watachuana vikali jukwaani, na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”, alisema Upendo.

Amesema kuwa kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh 25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=. 

Kwa upande wa Burudani,Upendo amesema kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli, Muziki wa Asili, Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine  mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: