Historia imewekwa leo na Flaviana Matata alipokabidhi msaada wa maboya (life vests) 500 kwa Shirika la Meli la Taifa (Marine Services Co Ltd) kama sehemu ya kumbukumbu ya MV Bukoba - ambapo ni miaka 16 tangu Meli hiyo ilipozama na kuua watu takriban 1,000 akiwemo pamoja na mama yake Flaviana.
Waombolezaji wengine waliofiwa na ndugu zao wakiombea marehemu wa ajali hiyo.
---
Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kuokolea maisha ya watu katika vyombo vya usafiri wa majiambavyo vimelengwa maalum kwa Ziwa Viktoria mjini Mwanza. Msaada wa vifaa hivyo umeelekezwa katika shirika la kiserikali la usafiri wa majijijini Mwanza lijulikanalo kama Marine Service Co. Ltd.
Flaviana Matata ametoa jumla ya vifaa hivyo 500 (vyombo vya kuokoleamaisha ndani ya maji) ikiwa ni kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MvBukoba mnamo Mei 21 mwaka 1996 ambapo pia alimpoteza mama yake mzazi katika ajali hiyo iliyouwa watu takribani 1,000.
Sababu mojawapo kubwa iliyofanya watu kupoteza maisha yao siku ya tukio hilo ilikuwa upungufu na ukosefu wa vifaa vya majini kama maboya (Live Vest).
Toa Maoni Yako:
0 comments: