Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mwenye Dhamana ya Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mahojiano na Clouds Fm 88.4 Dar es Salaam kuelezea mambo machache yanayohusu Muungano. Pia ujio wake ndani ya Clouds Fm ni kuelezea changamoto zinazokabili Tanzania Bara na Visiwani inapotimiza miaka 48 tokea nchi hizi mbili zimeungana, changamoto ya kwanza ambayo Waziri amezungumzia ni ile ya mfanyabiashara kununua bidhaa Zanzibar wakija huku Tanzania Bara TRA nao wanatoza tena kodi, kama kwamba ametoka nchini nyingine. Suala lingine ni gawio la BOT kupata 4.5% ya gawio zima. Mengi zaidi unaweza kusikiliza Jahazi la Clouds FM na vipindi vingine vyote.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mwenye Dhamana ya Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na muandaaji wa Jahazi la Clouds Fm, Simalenga Simon.
Toa Maoni Yako:
0 comments: