Mmoja wa Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha
Dodoma (UDOM) akishusha Baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi wakati
wanafunzi wa UDOM walipowasili Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo
Manispaa ya Dodoma Mjini mchana wa leo.
Mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma
Areman Kaziguto (mwenye fulana nyeupe) akitoa maelezo machache mbele ya
wanafunzi wa shule ya sekondari ya viwandani iliyopo manispaa ya Dodoma
mjini ambapo wanafunzi wa UDOM leo walifanya ziara na kukabidhi msaada
wa vifaa vya kufanyia Usafi
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Viwandani ambao ni wanachama wa klabu ya mazingira shule hapo wakiwa
makini kusikiliza somo lililotolewa juu ya umuhimu wa kutunza mazingira
mchana wa leo
Picha hapo juu ni Mwanafunzi wa UDOM
Josephat Lukaza akitoa Maelezo jinsi
ya matumizi sahihi ya vifaa vya kufanyia na kutunzia uchafu kwa
wanafunzi
wa klabu ya mazingira ya shule ya sekondari ya viwandani iliyopo Dodoma
mjini
Wanafunzi wa Klabu ya Mazingira ya
Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo mjini Dodoma wakisikiliza kwa
makini baadhi ya maelezo kutoka Kwa Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM) mchana wa leo.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha
Dodoma wakiwa makini kusikiliza Wanafunzi wa Klabu ya Mazingira
Wakichangia Mada mbalimbali kuhusu Umuhimu wa Kutunza mazingira wakati
walipotembelewa na Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) leo
mchana
Mwenyekiti Wa Klabu ya Mazingira ya
Shule ya Sekondari ya Viwandani Idrisa Ramadhani akitoa shukrani kwa
wanafunzi wa UDOM waliotembelea shuleni hapo na kutoa msaada wa vifaa
vya kufanyia usafi
Mwalimu wa Klabu ya Mazingira ya
Shule ya Sekondari ya Viwandani Bi Ester Bahati akitoa shukrani za dhati
kwa wanafunzi wa UDOM waliotembelea Shule hiyo na Kutoa Misaada ya
Vifaa vya Kufanyia Usafi leo Mchana
Wanafunzi wa Klabu ya Mazingira ya Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo kwenye manispaa ya Dodoma wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) waliotembelea Shule hiyo Mchana wa leo. Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog - http://josephatlukaza.
Toa Maoni Yako:
0 comments: